Kura Yangu Nilimpa Rais Magufuli,Lakini Kwa Sasa Naijutia

Binafsi wakati wa kampeni nilivutiwa sana na sera ya Rais Magufuli ya kuipunguza serekali yake kwa nia ya kubana matumizi.
Na nia yake hiyo njema kwa taifa masikini Kama Tanzania ndio ilinishawishi nikiri nikampa kura yangu ya ndio.

Ila kwa sasa nimeanza kukata tamaa kwa uteuzi aliofanya Rais wa kuteu makatibu wengi watakao turudisha pale pale tulipokuwa tunalia lia kuwa serekali ni kubwa mno na isiyokuwa na mashiko.Inayoumiza wananchi wake.Ni kiri wazi nimeanza kuijutia KURA yangu na next time Ccm sitowaamini tena na siwaamini tena hata sasa hivi.

By Kibo10

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. uwiiiii tobaaaaa... na wengine nimewasikia wakisema hivyo pale jangwani baada ya nyumba zao kuchorwa X. mbona mapema sana kujuta bado hujaisoma namba.

    ReplyDelete
  2. Mume anaepata kibali toka kwa Mungu cha kuoa wake wanne,na tena kwa kuwachagua mwenyewe bado hawezi kuwaridhisha wote kwa kuwapa huduma na mapenzi sawa,sembuse Magufuli mwenye kubeba raia zaidi ya milion 45...,Pole wewe na ukawa yako.HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  3. Huo ni muendelezo wa kiwewe ulichopata mara baada ya kusikia matokeo na kwamba JPJM ndio rais.pole sana.

    ReplyDelete
  4. Subiri 2020
    Hapa kazi tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad