Kutorushwa Kwa Bunge Live kupo Pale Pale- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Majaliwa
Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Hai ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe aliyetaka kujua kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi wasione matangazo ya Bunge moja kwa moja.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.

''Maamuzi ya chombo hiki yameungwa mkono na serikali na waziri Nape Nnauye amefanya kipindi maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi maalum usiku'' Amesema Waziri Majaliwa.

Aidha chombo cha umma kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wa maswali na majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kurushwa katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wanaNCHI BANA MIMI NIPO KAZINI LIVE YA NINI LIVE NI REDIONI TU

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...Hongera dola KWA msimamo thabiti.

    ReplyDelete
  3. minafiki utaijua tu, kama wewe uko kazini na huitaji sikiliza hilo ni lako, wengine tupo kazini na tuna muda huo wakufuatilia, na kazi hazifanani! tunataka live, wanaogopa nn kuweka live.

    ReplyDelete
  4. Hawa wote wanaounga mkono upuuzi wa nepi aidha hawajitambui, au ni misukule ya fisiem!!!!

    ReplyDelete
  5. Na sherehe za CCM hatuzitaki kuonyeshwa Na TBC
    Lazima ccm yalivyo majizi yataonyesha huko huko
    Na nyinyi wafanya kazi wa TBC poleni kuongozwa nape

    ReplyDelete
  6. Asinge die nywele huenda angekuwa Na akili timamu
    Mtu mzima ovyo Kwani nywele yeusi ndo akili

    ReplyDelete
  7. poa tuu kuna vitu kibao serikali inatakiwa kuviangaikia umeme maji dawa mahospitalini walimu wakutosha mashuleni hili la bunge live sioni haja nalo
    kwanza hizo pesa zilikuwa zinaenda kwa watu mifukoni tuu mwa watu bunge mchana hakuna kama hutaki hama nchi

    ReplyDelete
  8. Haja ya live ni watu kujitafutia sifa za kubwabwaja ili wapate kiki bila ya kuzingatia taratibu. Naaiaitiza live haina afya zaidi ya miubishi ya mijisifa. Hapa ni kuchapa kaz kwa busara kutengeneza kik hakuna nyambaf......

    ReplyDelete
  9. KAMA ILIVYOKUWA NGUMU KWAKO KUJENGA HOJA NDIVYO ILIVYO NGUMU KUPAMBANUA HOJA ZINAZOJADILIWA BUNGENI. HIVYO KWAKO BUNGE HALINA MAANA!BUNGE NDO LINATUNGA SHERIA HIVYO NI JUKUMU LA KILA MTANZANIA KUJUA KINACHOENDELEA HUKO ILI USIJEKUTA UNAVUNJA SHERIA BILA KUJUA KWANI KUTOJUA SHERIA HAKUNA EXCUSE.

    ReplyDelete
  10. Acheni upuuzi, hao waingerza na wajerumani hawana live kutoka bungeni na wapo vizuri kiuchumi. Kuona live kutoka bungeni inasaidia nini kimaendeleo? huu ni muda wa watu kufanya kazi. Hata nchi ya Japani haina live ya bunge na utambue asilimia 85 ya magari tunayomiliki nchini yanatoka nchi hiyo. Huu ni wkati wa watanzania kufanya kazi badala ya kuangalia wabunge wakibishana kuondoka nje ya bunge kama sasa. Siku zilizopita tulikuwa tunapata habari za bunge kupitia radio kabla ya TV na mambo yalikuwa mazuri tu.Watanzania tuache uvivu tufanye kazi tuwaachie tuliowaamini kutuwakirisha huko. ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau WaTZ tunapenda mkato sana,kwa watu wa magazeti walitakiwa wafurahie uamuzi huu maaana kwa kibiashara ndio wangekua na kwamba hata ununuzi wa magazeti ungekua kuliko hivi sasa.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad