Kwa Hili la Samatta, Serikali Inafanya Double Standards...Mbona Diamond Hajawahi Fanyiwa Sherehe wala Kupewa Zawadi na Serikali?

Wapendwa wanajukwaa na watanzania kwa ujumla, ni dhahiri kwamba sote tunapenda kuona nchi yetu ikisonga mbele kitaifa na kimataifa katika michezo na sanaa mbalimbali. Tumeshuhudia baadhi ya vijana wetu wakifanya vinzuri kimataifa na kuiletea heshima tele nchi yetu.

Sasa pamoja na heshima hii nina jambo ambalo naliona hakika halijakaa sawa na pengine linaleta picha mbaya kwa wananchi kuanza kudhani labda ni michezo au sanaa za aina fulani tu ndizo ambazo serikali inazithamini. Ni wiki iliyopita ambapo tumeshuhudia mchezaji wa soka Mbwana Samatta akitangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika. Tumeshuhudia namna serikali ilivyomtembeza mtaani kama kumpongeza kwa tuzo aliyopata. Leo hii muda huu Vodacom na serikali wameandaa hafla ya kumpongeza kwenye Hotel ya Hyat Regend. Kwa mujibu wa posts zinazowekwa na Vodacom katika mtandao wa instagram ni kwamba Samatta amepewa zawadi na serikali pesa taslim na kiwanja huko Kigamboni. Napongeza kwa hilo ni jambo jema hasa katika kutia moyo.

Sasa hoja yangu inakuja hapa, je serikali inayatambua mafanikio ya mpira wa miguu peke yake na si sanaa zingine pia? Nasema hivi nikichukulia mfano Diamond Platinumz. Hakuna mtu asiyetambua mafanikio aliyopata Diamond katika muziki kiasi cha kuiletea heshima kubwa nchi yetu katika Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Mbali na tunzo nyingi alizopata Diamond katika Afrika hii, ameweka historia ya kuwa msanii wa kwanza Afrika kushinda tunzo ya dunia inayotolewa na MTV. Ni msanii aliyewafanya waafrika na dunia kwa ujumla waanze kujifunza na kukielewa kiswahili hasa kutoka na nyimbo zake kutumia kiswahili na hata katika nyimbo anazoshirikishwa nazo anaimba kwa kiswahili. Ni msanii aliyefanya soko la mziki wa Tanzania likabadilika hasa katika suala la malipo wanayopewa wasanii katika matamasha na shoo wanazoalikwa. Ni mwanamuziki pekee wa Tanzania aliweza kuzivuta media za kimataifa kama BBC, Aljazeera na CNN kuweza kufanya naye interview.

Pamoja na mafanikio yote hayo hakuna hata kiongozi mmoja aliyediriki kumpa hongera Diamond kwa tunzo kubwa ya Dunia aliyoipata. Nimejiuliza sana na kudhani labda michezo na sanaa zinazothaminika na serikali ni mpira wa miguu tu.


Udaku Special Blog

Post a Comment

45 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. True brother haipo sawa

    ReplyDelete
    Replies
    1. umbuka slogan ya awamu ya tano'hapa kazi tu'sio maisha bora kwa kila mtanzania.so mwambie diamond wako afanye mambo naye atafanyiwa sherehe na kupewa zawadi.acha kuchonganisha watu.

      Delete
    2. umbuka slogan ya awamu ya tano'hapa kazi tu'sio maisha bora kwa kila mtanzania.so mwambie diamond wako afanye mambo naye atafanyiwa sherehe na kupewa zawadi.acha kuchonganisha watu.

      Delete
  2. we unaonaje mtoa mada kulisakata kabumbu mpaka kieleweke na kunengua na kuimba maloloso jukwaani ipi ni heshima kwa taifa? soka ndio ya kujivunia ndio maana kuna kombe la dunia. pig up samatta mwenye wivu ajinyonge!!!

    ReplyDelete
  3. mziki umezoeleka na vijana wengi wameuelewa na wanaufanya kiushindani na hata hivyo familia nazo zina sapoti mziki kwahiyo mziki bongo umeshainuka
    mpira bado haujawa kivile bongo na samatha ni kama kafungua mianya soo serikali si mbaya ikimpa nguvu samatha kwa manufaa ya kuinua soka la bongo na kulipeleka soka letu kimataifa zaidi
    ila naule ubabe na umafia wa TTFF serikali nayo iingilie kati coz wanachangia kudumaza soka la bongo
    kama samatha angeendelea kubaki simba sidhani kama angefika apa alipofika sasa
    hongeraa samatha endelea kukaza buti bado tunakutumainia

    ReplyDelete
  4. 😂 😂 😂 😂 😂 😂 lol tuzo zake hazina mvuto nyingi mno alafu hii tuzo ya samata kiboko soccer puts a country on the map, alafu yeye anaingia tuzo nyingi mno zingine hata hazijulikani ndo maana ,yaani kuna nyingine hata ukiwa nominated ni dili hizo zake za wanaijeria haaaaah lol 😂 😂 😂 mungu nisamehe but that's is the truth

    ReplyDelete
  5. Yaani umeongea pumba kabisaaaa

    ReplyDelete
  6. Yaani umeongea pumba kabisaaaa

    ReplyDelete
  7. Yaani umeongea pumba kabisaaaa

    ReplyDelete
  8. Chizi kweli wewe muandishi

    ReplyDelete
  9. Diamond ndio nani kwa Samata?

    ReplyDelete
  10. Diamond ndio nani kwa Samata?

    ReplyDelete
  11. Udaku nomaaaa hamna jema,,,,Diomond ni Diomond na Samanta ni Samanta,,,,,wakati wa Diomond Nape alikua Waziri? Hamna jema walimwenguuu

    ReplyDelete
  12. Diamond ndio nani kwa Samata?

    ReplyDelete
  13. Mpira wa miguu Una timu ya taifa ambayo Mara kwa Mara hushindwa kimataifa. Sasa huyo mama kashinda kwa nini asipongezwe kuhamasisha wachezaji wadogo waongeze bidii ili timu yetu ipate wachezaji wazuri kutuwakilisha kisoka? Huo mziki Una band ya taifa mpaka serikali impongeze? Muziki Ni mtu binafsi. So hata nyie media mkimpaisha mwanamuziki aliyeshinda kimatsifa inatosha. Acheni vijana wenye vipaji vya kusukuma kabumbu wahamasishwe kupitia samatta.

    ReplyDelete
  14. Hii maana yake muziki unabagua,lakini mpira wa miguu unapendwa na watu wa rika lote,kwa kile kilichofanyika na serikali ni kufurahisha watanzania wote kwa kuona tuzo ya Samata.Tulikaa sebuleni na wazazi kuangalia nani atachukua tuzo na tulipisikia Samata anatajwa wote tulilipuka kwa shangwe,lakini sijawahi kuona wazee wangu wanangoja kuona ushindani kwa upande wa muziki.

    ReplyDelete
  15. Hongera samatta, suala la serikal labda useme zawad ila mbona dai kaoneshwa sana kua recognazed mpk kuitwa ikulu

    ReplyDelete
  16. we adm bwege kweli, unataka serikali imfanyie diamond sherehe kwa yeye kufanya nini? kukata viuno jukwaani?

    ReplyDelete
  17. wanga huwa hamna jema sasa ndo unataka mond naye apewe au

    ReplyDelete
  18. bahati ya paka si bahati ya mbuzi

    ReplyDelete
  19. Kuna mashehe,wachungaji na taasisi nyingi hazitaki kusikia muziki wa dunia lakini wanapenda mpira,viongozi wanaangalia nini kinawakuna watanzania wote.YES!ni mpira wa miguu,angalia hata uwanja unavyojaa wakati wa mechi hasa za kimataifa,wazee,wanawake,watoto wote utawaona uwanjani,na sio TZ tu ni kote duniani.
    Jiulize au umeshawahi kuona RANKING kwenye muziki?

    ReplyDelete
  20. kwa sasa ni serikali mpya, waziri mpya na mkakati mpya. so usilaumu make kila mtawala na mipango yake. ndiyo maana wasanii wataanza kulipwa na studio. zamani ilikuwepo?

    ReplyDelete
  21. Uko sahihi mdau kuna upendeleo hapo sana

    ReplyDelete
  22. acheni uchochezi hii ni serikali ya awamu nyingine nao wana mikakati yao

    ReplyDelete
  23. atapewa tuzo na kina wema sepetu, mwandishi kuma wewe

    ReplyDelete
  24. Well said! Naona Nape amekurupuka. Ameona ndio assignment yake kubwa ya kwanza tangu awe Waziri. Diamond anastahili zawadi×10!!!

    ReplyDelete
  25. Serikali haitoi wala kutoa heshima watu ambao wana scandaly kila kona
    Si wadilifu
    Waropaji
    Wanaangalia maadili
    Domo kazidi mdomo
    Dharau
    Hata baba yake mzazi japo ni private matter

    ReplyDelete
  26. wewe mwandishi acha uchochezi tumia kalamu yako

    ReplyDelete
  27. SAMATHA ;meulleur joueur africain ...loko..SIOJAMBO LA KITOTO
    UYO DAIMOND ANANUNUWA TUZO AMNA KITU
    WA TZ JUWENI KUTOFAUTISHA

    ReplyDelete
  28. assume ndo wameanza na sammata acha longolongo nyingi

    ReplyDelete
  29. Dai kazidi kusijisia na kutukana maa x wake. sasa serikali impaishe nn.

    ReplyDelete
  30. Serikali inajua fika Dai anahonga ili nyimbo zake zipigwe na zawengine ziwe chini yake ndo maana.

    ReplyDelete
  31. Almasi anaroho mbaya kwa wenzie anahonga ili awe juu, sasa unafikri serikali haijui

    ReplyDelete
  32. kweli huyu muandishi uchuro anashindwa kuchanganua mambo ya nyakati anyways unaposoma gazeti la udaku usishangae kukutana na habari zisizo za maana kama hizi.hii ni serikali ya magufuri ina waziri wa michezo anayetaka ku proof anasimamia kazi yake je kipindi cha diamond ilikuwa serikali ya nani

    ReplyDelete
  33. kweli huyu muandishi uchuro anashindwa kuchanganua mambo ya nyakati anyways unaposoma gazeti la udaku usishangae kukutana na habari zisizo za maana kama hizi.hii ni serikali ya magufuri ina waziri wa michezo anayetaka ku proof anasimamia kazi yake je kipindi cha diamond ilikuwa serikali ya nani

    ReplyDelete
  34. Domo awezi kupewa heshima kama ya Samatha, anahonga ili apate tuzo hamshangai eti Emola sijui nani yule anaeishi nae kawa wa 3. yaani anajipaisha na mto anaemtaka anafikiri atakuwa juu miaka yoote.

    ReplyDelete
  35. Dai aendelee kuhonga awe juu tuzo zenyewe hazina mshiko na azidi kuwabania wengine lakini cku zake zitafika hasidi mkubwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. duu mdau ona aibu hivi unaweza ukahonga MTV???

      Delete
  36. Kachelewa kupata tunzo angepata mapema ccm wangemtia kwenye kampeni za uchaguzi

    ReplyDelete
  37. Hizo za muziki hata Vanessa Mdee kesha chukua....no deal. Hongera sana Sammata

    ReplyDelete
  38. Who is Diamond kwani, samata deserves kabisa muachie kutuchafulia furaha mfyuu

    ReplyDelete
  39. sasa nimejua kwanini watanzania ni masikini.

    ReplyDelete
  40. SIO DIAMOND PEKEE HATA VANESA MDEE, JIDE, NA WENGINE WALIOPATA TUNZO ZA KIMATAIFA.

    ReplyDelete
  41. Si anatamba kika kona ana majumba ubishoooooo unamsumbuwa na ulimbukeni
    Awamu nne wakwere wenzie ndo maana alikaribishwa ikulu
    Awamu tano hata apate medali kwa queen Hana maadili domo
    Ana dharau, kujisikia
    Shule Kweli hazina

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad