Kwa hili lazima tuseme, kwamba kama mwanachama halikunifurahisha hata chembe.
Ni jambo lililo wazi kuwa baada ya uchaguzi mkuu, CCM tumepigwa bao hasa hapa jijini Dsm.
Halmashauri nyingi waliochaguliwa ni wanachama wa vyama vya upinzani kwa wingi zaidi kuliko wa chama tawala.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kiuhalisia.
Dhambi kubwa na ya kutia aibu, ni kuleta mamluki toka Zanzibar, watuamulie mambo ambayo kwanza hawayajui ya DSM, na pili si wawakilishi wa wananchi wa DSM.
Katika kata yangu, diwani alichaguliwa wa CHADEMA, mimi nilimpa kura yangu(wa CCM) alishindwa vibaya.
Kushindwa kwa huyo mwana CCM mwenzangu kunatokana na kutoshughulikia kero , hasa za barabara huku Mbezi.
Sasa leo huyu mwana CHADEMA TUTAMPIMA KWA KIGEZO HICHO HICHO.
Sasa leo tunaletewa mamluki wa kutusaidia kuamua mambo yetu?
Mbaya zaidi ni kususia uchaguzi.
Hii ni AIBU KUBWA!
Toa maoni yako
na bado hata urais mliiba kura
ReplyDeletefyuuuu ccm
nape sema basi na haya