Kwanini "Service Charge" ya TANESCO ni Tatizo Linalohitaji Utatuzi Haraka...!

Najua watu wengi wameandika kuhusu Tanesco na naomba kwa wasimamizi wa Jukwaa hili wauache uzi huu kama ulivyo ili wahusika (ambao nina hakika watausoma) wapate kujua kwa kina.

Kwanza kabisa kwa wale wanaotumia umeme wanajua kwamba tulikuwa na mfumo wa zamani ambao Tanesco walitembelea nyumba zetu na kufanya matengenezo na ukaguzi wa mambo mbalimbali ikiwamo mita za umeme. Sina hakika kama hichi ndio chanzo cha haya makato, lakini ni dhahania yangu kuwa ndizo "service" tulizolipia nyakati hizo.

Sasa ni nyakati mpya. Ukitaka LUKU unalipia, na umeme unaotumia pia unalipia. Sasa service charge ni za nini? Service ipi hasa ambayo unatozwa wakati mwingine mpaka 5000/= au zaidi kwa mwezi?

Hebu tulinganishe makato haya kuona tatizo hili jinsi lilivyo kubwa:
Ukiwa na akaunti ya kawaida benki unalipia kama 700/= kwa mwezi. Ukiwa na akaunti ya kampuni, unalipia kama 7000/= kwa mwezi. Ukiwa na LUKU unalipia kama 5000 kwa mwezi.

Nadhani hata neno LUKU halina maana hapa. Kwa sababu LUKU ni lipia kadri unavyotumia. Naomba niweke mifano miwili tu hai kuonyesha tatizo hili sio dogo kama wengi wanavyolichukulia:
Kuna watu wawili hawakuwepo nyumbani kwa miezi 6. Mmoja alinunua umeme wa elfu 60 na mwingine elfu 50. Wa elfu 60 alipata unit 0 na wa pili alipata unit zisizofika 10.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wanatumia umeme husika kwa miezi yote sita. Iko wapi hapo concept ya Lipia Kadri unavyotumia?

Lakini katika makato hayo kuna makato ya REA. Ni makato yenye lengo jema kabisa, kusaidia kupeleka umeme vijijini ili kusukuma maendeleo. Hivi tukiwa wakweli, watu wangapi vijijini wataweza kulipia 5000/= au zaidi kwa ajili ya "service charge"?

Kabla sijamalizia naomba kuelimishwa kwa nini umeme una makato mengi hivi ilhali ndiyo primer energy kwa maendeleo yetu? Kwanza bei ya umeme wenyewe kwa unit ni mkubwa sana (295/= kwa unit). Hapo bado kuna VAT (18%), EWURA (1%), REA (3%) na service charge (5000+/= @month).

Nadhani ni wakati wa kutuondolea haya makato. Mtu anayehitaji Tanesco service na ailipie kwa wakati huo atakapoihitaji. Haya makato ya kiujumla jumla tu yanaumiza sana wananchi. Niisihi serikali iliangalie hili kama moja ya mambo yanayorudisha nyuma sana maendeleo yetu. Umeme ni nishati muhimu sana na hivyo ni vyema ikaangaliwa kwa ukaribu kabisa ili kuleta mapinduzi ya kiteknolojia.

By Stefano Mtangoo

Udaku Special Blog
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu Ni wizi wa moja kwa moja nachukia Sana hizi hidden cost ambazo hazina maelezo yasiyonyooka tuelezeni tanesco service for every month mmeitowa wapi na kwa mashiko yapi?

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli huu ni zaidi ya uonevu,,LUKU yangu,umeme nanunua, kodi unakatwa, Service charge ya nini?...

    ReplyDelete
  3. Service charge analipwa bw.Mamvi kwa mkataba wake mbovu na Tanesco wa Richard monduli.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad