Lowassa, Maalim Seif Waishika Zanzibar..Ukawa Kutoa Tamko Zito

Lowassa na Maalim Seif
Zanzibar. Siku moja baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) kuitangaza Machi 20 kuwa siku ya marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, mgombea urais, Maalim Seif Sharif Hamad na Edward Lowassa leo wanakutana na wabunge wote kutoka vyama vinavyounda Ukawa kutoa “tamko zito” litakalotoa mwelekeo wa hali halisi ya kisiasa visiwani humo.

CUF, ambayo inapinga kurudiwa huko kwa uchaguzi, nayo imepanga kufanya vikao vyake vya juu mapema wiki ijayo kuweka msimamo wake kuhusu tangazo hilo.

Wakati hayo yakiendelea, mabomu ya machozi jana yalilipuliwa kwenye maeneo tofauti ya Zanzibar wakati askari wa Jeshi la Polisi wakitawanya watu waliokuwa wamekaa kwenye vikundi, kwa kuhofia kuwa wanaweza kutumia mwanya huo kufanya vurugu.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alitangaza juzi kuwa marudio ya uchaguzi hayatatanguliwa na kampeni za wagombea wa nafasi za urais, uwakilishi na udiwani na wala hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya wagombea.

Bado vyama vya upinzani havijatoa tamko kuhusu uamuzi huo wa ZEC, lakini viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa; Chadema, CUF, NLD na NCCR Mageuzi wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa African Dream.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. .magazeti aina hii ha yatakuwa kwenye jamii ya naleta uchochezi wa Hali ya juu. Ebu waziri mwenye dhamana a Liang a lie ili gazeti kwa macho manne zaidi kabla ya kuleta adhari.

    ReplyDelete
  2. we kirenga MILEMBE wanakutafuta ukachuku dawa zako.

    ReplyDelete
  3. Waeni kijeshi Na nyinyi
    Bongo ruhusa mpambane nao
    Tumetochoka Na maneno
    Amani haipatikani ila kwa upanga

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad