Lulu: Tekno Alijigonga Kwangu..Na hivi Ndivyo Ilivyokuwa...

STAA wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameendelea kukanusha ‘ubuyu’ ulionea kuwa alivunja amri ya sita hotelini na msanii wa muziki wa Nigeria, Tekno Miles, akitoa maelezo yaliyotafsiriwa kuwa, kumbe mwanamuziki huyo ndiye aliyejigonga kwa mkali huyo wa sinema za Kibongo.

Lulu alilazimika kukanusha habari hizo kufuatia kusambaa kwa picha zake na jamaa huyo ambaye ni ‘hitimeka’ wa Ngoma ya Duro, zikiwaonesha wakiwa wamekumbatiana usiku wa Mkesha wa Mwaka Mpya 2016 ambapo Tekno aliangusha shoo ‘hevi’ kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar, kabla ya kudaiwa kwenda ‘kumbonji’ wote katika Hoteli ya Serena iliyopo Posta.

Hata hivyo, kabla ya kuenea kwa picha na habari ya Lulu na Tekno, chipukizi wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ naye alihusishwa na kulala na mwanamuziki huyo hivyo kuibuka kwa utata na maneno mengi yaliyolenga kuchochea bifu kati ya warembo hao wa Kibongo.

Ili kumaliza ubishi huo, Amani lilimpa nafasi Lulu ili kueleza kile anachokifahamu katika sakata hilo ambapo alifunguka: “Kama nilivyoeleza kwenye kurasa zangu za social media (mitandao ya kijamii), nasisitiza, nilikutana na Tekno kwenye shoo yake ukumbini.

“Yeye (Tekno) ndiye alikuja kunisalimia kwenye meza yangu na siyo mimi niliyemfuata. Nilikwenda kwenye shoo yake kama shabiki wake na siyo vinginevyo na picha alipiga na watu wengi si mimi tu.”

Chanzo: Global Publishers

Udaku Special Blog

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. akiendelea kujigonga mkanumbe. kama ulivyowakanumba komba na nani yule mbaba...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Koma wewe mwanga mkubwa
      Yaliyotekea kwa RIP kanumba
      Yanaweza kutokea hata kwako
      Aujuwaye ukweli ni mungu Na hao wawili
      Fyuuuuuuu
      Wivu tu

      Delete
  2. Hahahahaha,!!'!!!!!wabongo ni shida

    ReplyDelete
  3. bongo movie
    bongo lalalaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad