MAMILIONI ya shilingi ya Mamlaka ya Bandari (TPA), yaliyohifadhiwa katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), yamenusurika kukwapuliwa na baadhi ya vigogo serikalini.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na mkuu wa ulinzi na usalama, L.J. Twange, wizi huo ulipangwa kutekelezwa tarehe 24 Novemba mwaka jana.
Katika maelezo yake, Twange anasema, “…kugundulika kwa mpango wa kukwapua fedha hizo, kulijukana baada ya mtunza fedha wa Bandari ya Mtwara (Port Cashier), kufika katika tawi hilo na kuomba taarifa za fedha (balance) za mamlaka.
Anasema, “katika harakati za kuangalia salio, ndipo alipogundua kuwa kiasi cha Sh. 87,730,000 kimetolewa kutoka kwenye akaunti ya shirika.”
Mamilioni hayo ya shilingi yalipangwa kuchotwa kutoka kwenye akaunti Na. 034103000143, iliyopo benki ya NBC, tawi la Mtwara.
Maelekezo ya kuhamishwa kiasi hicho cha fedha yalipokelewa kwenye benki hiyo kwa barua ya 24 Novemba 2015, yenye Kumb. Na. AC/2/1/022/1153 iliyodaiwa imetumwa kutoka bandari makao makuu.
Kwa mujibu wa barua hiyo, fedha hizo ziliekelezwa kupelekwa kwenye akaunti Na. 33012228976 inayomilikiwa na kampuni ya KILAM Limited.
Akaunti ya kampuni ya KILAM iliyotaka kuingiziwa fedha hizo, iko benki ya KCB, tawi la Mlimani City.
Nyaraka ambazo MwanaHALISI Online imezinasa zinaonyesha, “kulikuwa na uharakishaji wa malipo ya fedha kwa kampuni ya KILAM Ltd.”
Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa na Juma Mwenda, mfanyakazi wa kampuni ya KILAM, kwenda kwa Nelson Mwaikyokile, meneja wa operesheni wa tawi, malipo hayo yalitakiwa kuhamishwa kwa haraka na bila kukosa.”
“Baada ya kushindikana kuhamishwa kwa fedha hizo kutokana na ufinyu wa salio, wahusika wa mpango huo wa uhalifu, walituma barua pepe nyingine siki iliyofuata (25 Novemba), kuomba kuhamisha kiasi cha Sh. 187.7 milioni kutoka kwenye akaunti hiyohiyo.
“Hata hivyo, uhamishaji huo nao haukufanyika kutokana na uhaba wa fedha kutoka kwenye akaunti hiyo inayotumika kwa ajili ya makusanyo,” ameeleza Twange katika taarifa yake yenye kurasa tano kwa mkurugenzi mkuu wa bandari amethibitisha kuwapo kwa wizi huo.”
Wizi mtupu!
ReplyDelete