Maskini Wastara! Majanga Yazidi Kumwandama...Nyumba zake Mbili kuvunjwa na Bomoa Bomoa...Apata Mshituko Mkubwa

Muigizaji wa filamu, Wastara Juma amejikuta katika wakati mgumu tena baada ya nyumba zake mbili kupitishiwa X kwaajili ya kubomolewa siku zijazo.

Katika ukurasa wake wake wa Facebook, Wastara ameandika:

Mashabiki wangu mwaka umeanza vibaya kwangu nyumba zangu mbili zimewekwa X na zitabomolewa siku yoyote kuanzia leo,siko sawa kabisa niombeeni dua presha imepanda,nawapenda sana

Akiongea na Bongo5, ndugu wa Wastara amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa hali ya muigizaji huyo si nzuri kutokana na mshtuko alioupata.

“Kweli Wastara hali yake sio nzuri amepata mshtuko baada ya watu wa mazingira kuweka X katika nyumba zake mbili,” alisema dada huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mariam uku akidai Wastara hawezi kuongea na simu.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole Sana dd wastara nakuonea huruma saana kutokana na majanga kukuandama,lkn hio ni sheria haiangalii uko vp au ww ninani,omba mungu ishaallah atakusaidia kuukunjua nafsi na utasahau yote yalokufika,Ila nakukimbusha tu kwamba ile kauli mbiu yetu ya HAPA KAZI TU,haichagui kwahio usijali sn ndio kauli mbiu yachama chetu,usisahau

    ReplyDelete
  2. Pole wastara.
    Hata mimi hili zoezi limenikumba,kwa kuwa ni amri na ni
    moja ya kuweka nchi sawa tukubali tu matokeo.Mungu ndiye mpangaji wa yote,yatapita.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad