Mbaba Atupwa Jela Miaka Mitatu Kwa Kunajisi Zabinti zake Wawili wa Kuwazaa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela, Abdallah Saidi Kundumu, mkazi wa Miembesaba wilayani Kibaha, baada ya kukutwa na hatia ya kunajisi mabinti zake wawili wa kuwazaa.

Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Aziza Mbadjo alisema kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2013 na 2015, hivyo kutokana na kifungu cha sheria 158, kifungu cha kwanza cha kanuni ya adhabu anapaswa kutumikia adhabu hiyo.

“Ushahidi umejitosheleza pasipo kuweka shaka, maana hii ni kesi ya Jamhuri na kabla ya kutoa hukumu tunazingatia ushahidi wa kuaminika unaojitosheleza kulingana na taratibu zinavyoagiza na nimejiridhisha, hivyo anapaswa kutumikia kosa hilo,” alisema.

Mwendesha mashitaka katika kesi hiyo Inspekta Rashird Chamwi alidai kuwa kwa mujibu wa maelezo kutoka baadhi ya majirani wamshtakiwa huyo, zilieleza kuwa amekuwa akiwafanyia vitendo hivyo mabinti zake wa umri wa miaka 15 ni mwingine miaka 11.

Alidai kuwa watoto hao baada ya kuchoshwa na vitendo hivyo vya baba yao, waliamua kumjulisha mama yao mzazi ambaye kulingana na shughuli zake za ujasirimali amekuwa akilazimika kuondoka nyumbani alfajiri, kabla watoto hawajaamka na kurejea usiku jambo ambalo limekuwa likimpa nafasi mzazi huyo wa kiume kutekeleza vitendo hivyo.

Alidai kuwa kutokana na hali hiyo majirani wa familia hiyo walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na kufanyika uchunguzi wa kina na kubaini kuwapo kwa ukatili huo, kwa kuzingatia sheria watoto hao walifanyiwa vipimo na kukutwa na athari ambazo zinasababishwa kufanyiwa vitendo hivyo.    

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Miaka mitatu tuu mbona kidogo mno mmmh hapo ipo namna

    ReplyDelete
  2. Wadau hilo jibaba mimi kiupande wangu nahisi angeozea jela huyu unyama ulopitiliza du ulale na mkeo akitoka kwenda kutafuta uwarudie hawa malaika wa mungu,hamu ya vipi hiyo laana mkubwa wewe

    ReplyDelete
  3. Naona hiyo kesi haijaisha hiyo miaka mitatu ni ya kumpa introduction ya gereza tu. Hukumu kwa kosa halisi bado.

    ReplyDelete
  4. Naona hiyo kesi haijaisha hiyo miaka mitatu ni ya kumpa introduction ya gereza tu. Hukumu kwa kosa halisi bado.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad