Membe Atoa Msimamo Wake Adai Hawezi Staafu Siasa...Aweka Wazi Anachofanya Kwa Sasa

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema hana mpango wa kustaafu siasa kwa sababu haina mwisho.

Pia, amesema kwa sasa anafanya kazi ya uandishi wa vitabu kwa lengo la kuwashirikisha na kuwarithisha Watanzania mazuri aliyonayo baada ya utumishi wake wa kisiasa wa miaka 35.

Membe alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Alisema anaandaa vitabu vinne vyenye maudhui tofauti. “Hilo la kuandika vitabu nimeshalianza, nina vitabu zaidi ya 265 nimehifadhi na kuvisoma katika maktaba yangu kuhusu mambo mbalimbali ya dunia, nami ninatengeneza vinne, muda ukifika nitatoa taarifa,” alisema Membe.

Waziri huyo aliyehudumu katika Serikali ya Awamu ya Nne katika wizara hiyo kwa miaka tisa, alisema kati ya vitabu anavyoandika viwili vitatoka mwaka huu.

“Kimoja cha maisha yangu, ni vitabu vizuri sana, nimekuwa mwanasiasa kwa miaka 35, nimejihusisha zaidi na masuala ya utatuzi wa migogoro barani Afrika... kitabu kingine kitahusu migogoro na Serikali za Afrika,” alisema.

Alitaja vingine kuwa ni kuhusu uongozi na cha mwisho kitahusu siasa za Tanzania kinachowalenga zaidi vijana kikieleza namna nchi inavyoweza kulinda heshima yake duniani.

“Nchi hii tumeirithi kutoka kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Yeye alikuwa mwana ukombozi halisi. Mwaka 1963 alianzisha harakati za ukombozi, Tanzania ikawa makao makuu ya nchi zote zinazopigania uhuru. Vyama vya ukombozi vikaweka makao makuu yake hapa, vingine vikaanzia harakati zake hapa,” alisema Membe.

Alisema sifa ya kwanza ya Tanzania duniani ni ukombozi na ilikuwa mwenyekiti wa nchi tano zilizokuwa mstari wa mbele katika ukombozi Kusini mwa Afrika.

Akizungumzia kuhusu hatima yake kisiasa, Membe aliyewania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM kabla jina la Dk John Magufuli ambaye sasa ndiye rais kuteuliwa, alisisitiza kuwa siasa haina mwisho.

“Tafsiri ya siasa ni mchakato wa namna ya kuyashughulikia matatizo ya watu, usipoyashughulikia vizuri, utaibadilisha siasa kutoka kwenye amani kwenda kwenye mtafaruku,” alisema.

Akimnukuu aliyekuwa Rais wa Marekani, Bill Clinton, Membe alisema mwanasiasa mzuri duniani ni yule aliyeondoka kwa heshima na anayeheshimu familia yake.

Membe aliwataka wanasiasa walioshindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kuacha kujipenyeza na kuendeleza ubabe wa kisiasa, akisema kufanya hivyo ni sawa na upuuzi, badala yake wasubiri muda wao watakapochaguliwa. 

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu membe inaelekea lengo lake ni kujijenga ndani ya ccm lakini kwa ukosoaji MKALI unayemlenga mheshimiwa rais wa awamu ya tano john pombe magufuli ili ajaribu kujitengenezea njia ya kugombea urais kwa tiketi ya ccm 2020 jambo ambalo ni ndoto kwa mfumo wa mazoea na utaratibu usio rasmi wa ccm,magufuli atapitishwa na kuruhusiwa kugombea kwa awamu ya pili.sasa anachokifanya kuropoka-ropoka,kunaweza kumfanya achukuliwe hatua za kinidhamu na chama chake,na kwa kuwa ana makosa ya kinidhamu huko nyuma,WATAMFUKUZA.aende wapi?labda aanzishe chama chake kipya.unajua membe ni mroho na mwenye uchu mkubwa wa kuutafuta urais,ni mwehu-siasa asiye na uungwaji mkono pengine hata na mkewe.ni kichaa-madaraka.kwenda upinzani? membe si mtaji,ni garasa.hafai hata kwa kuumangia[kula ugali bila mboga].tatizo ninaloliona ni uoga wa serikali kumchukulia hatua za kijinai kwa uhalifu alioufanya akiwa mtumishi wa umma mwenye dhamana-waziri.wizi mkubwa wa fedha za gaddafi.inawezekana vipi kimfumo hapa duniani membe akabidhiwe yeye na sio serikali mamilioni ya dola za kimarekani?kwa misingi ipi?tatizo kubwa sana na zito kwa ccm ni kwamba ki-madhambi wanalindana sana sana.wee mwaga ugali uone,mi ntamwaga mboga.anatamba mhalifu asiyekamatika BERNARD MEMBE.

    ReplyDelete
  2. MAKALA FUNGAKAZI.

    ReplyDelete
  3. Watu wa nje aliowatetea wanamsukuma. Hupati kitu. Hamia huko wakupe cheo nchini kwao kama watakujali. Wakuchukue huko badala ya kukutumia uwahadae tena Watanzania. Akili mali.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad