Mengine Yaibuka Kuhusu Mbwana Samatta Kwenda Kucheza Ulaya..Aamua Kurudi TP Mazembe

Mbwana Samatta Akianya yake
Baada ya dili la uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta kusuasua kutoka klabu yake ya TP Mazembe kwenda klabu ya Genk ya Ubeligiji, star huyo ameamua kurejea kwenye klabu yake hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya mazungumzo na tajiri wa Mazembe Moise Katumbi kuhakikisha dili hilo linakamilika.

Manager wa Samatta Jamal Kisongo amesema, mbali na mazungumzo, Samatta amerejea kwenye klabu yake ili aendelee kujifua hata kama ikitokea boss huyo akamfungulia mlango wa kutokea basi awe yuko fiti kuingia moja kwa moja kwenye timu kuliko kuendelea kukaa nyumbani.

“Tumeona ni vyema Samatta akarejea Mazembe katika kumpa presha na kumsukuma Katumbi, amerejea kwenye kituo chake cha kazi na kumpa taarifa Katumbi kuwa kama hato muuza kwenye klabu ya Genk basi yeye atamalizia mkataba wake TP Mazembe na ataondoka mwezi April. Jambo ambalo kwa hakika Katumbi hawezi kukubaliana nalo kwakuwa anajua Samatta akiondoka mwezi April ataondoka bure na yeye atakuwa ameingia hasara”, amesema Kisongo  leo asubuhi wakati akihojiwa kwenye kipindi cha michezo cha E-FM Radio.

“Lakini tumeona pia ni muhimu akaenda Mazembe ili awe anafanya mazoezi hata kama ikitokea ameuzwa basi anaweza kutumika moja kwa moja kwasababu atakuwa yuko fiti”.

“Mkataba wake na Genk unampa nafasi ya kujiunga mwezi January kama Katumbi atamuuza, kama Katumbi atagoma, mkataba wake huohuo unampa nafasi ya kuweza kujiunga katika majira ya joto (mwezi wa 7)”.

“Mbwana Samatta jina lake halijaingizwa kwenye orodha ya majina ya wachezaji watakaocheza michuano ya klabu bingwa Afrika mwaka kuu, Katumbi alishamuacha kwasababu anajua anamaliza mkataba mwaka huu na atamuuza January. Kwa maana hiyo Mbwana hana faida kwenye klabu ya TP Mazembe kwasababu ligi ya ndani ndiyo ligi pekee anaweza kucheza ambayo hata wachezaji wengine wanaweza wakacheza vizuri tu”.

Mara baada ya Samatta kupata timu ambayo imeonesha kumuhitaji, boss wa Mazembe amekuwa akitia ngumu kumuachia Samatta kutimkia Ubeligiji badala yake amekuwa akimtafutia timu yeye mwenyewe huku akiwa na sababu zake binafsi za kufanya hivyo lakini hana sababu za kimantiki za kumzuia mchezaji huyo kujiunga na Genk.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwani tff haiwezi kusaidia hapo jamani????????

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad