KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kasi ya utendaji kazi ya Rais John Magufuli inaweza kuua uwepo wa vyama vya upinzani nchini.
Hata hivyo alisema kuwa hangependa upinzani ufe kwa vile hiyo pia itakuwa imeua demokrasia nchini na kudai kuwa lengo la kuanzisha vyama vya siasa haikuwa kuviua bali ni kuviona vikiendelea kuwepo.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu huyo wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya miaka 39 ya CCM ambayo kilele chake kimepangwa kufanyika mkoani hapa Februari 6, mwaka huu badala ya Februari 5 iliyozoeleka.
Alisema kuwa chama kimelazimika kubadili tarehe ya kilele ili kuwawezesha wananchi kushiriki ipasavyo maadhimisho hayo kwa kufanya kazi badala ya kuwa na sherehe mbalimbali.
“Maadhimisho ya safari hii ni tofauti na ya miaka mingine. Safari hii wananchi watatakiwa kushiriki zaidi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo. Kauli mbiu yetu ni ‘Sasa kazi’ hivyo watu wafanye kazi ili wajiletee maendeleo yao wenyewe,” alisema.
Nape Nnauye: Kasi Ya Rais Magufuli Itaviua Vyama Vya Upinzani Hapa Nchini
5
January 23, 2016
Tags
huyu jamaa ajui anachoongea
ReplyDeleteYa kuvaa nguo za jeshi wakati si mwanajeshi
ReplyDeleteFyuuuuuuu
Angalia waziri wa ulinzi alivaaa nini
Kama angekwenda vitani angevaa nguo hizo siyo kwenye mahafari
Pumbavu washauri wa rais Na CCM
mgeni rasmi akienda kwenye mahafari ya chuo na yeye anakuwa ana graduate?
Deleteakili za kuambiwa ongeza na zako shoga wewe la ukawa
Nape inaonekana unawashwa sana na upinzani?wakati wa kampeni umeisha boya wewe fanya kazi,wabongo wanawaangalia tu speed zenu hawataki sikia longolongo.
ReplyDeleteCCM mbele kwa mbele
ReplyDeletesema baba nape ni kazi yako kusema
cheo chako kinarusi katibu wa itikadi na uenezi