Nape Nnauye: Kasi Ya Rais Magufuli Itaviua Vyama Vya Upinzani Hapa Nchini

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kasi ya utendaji kazi ya Rais John Magufuli inaweza kuua uwepo wa vyama vya upinzani nchini.

Hata hivyo alisema kuwa hangependa upinzani ufe kwa vile hiyo pia itakuwa imeua demokrasia nchini na kudai kuwa lengo la kuanzisha vyama vya siasa haikuwa kuviua bali ni kuviona vikiendelea kuwepo.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu huyo wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya miaka 39 ya CCM ambayo kilele chake kimepangwa kufanyika mkoani hapa Februari 6, mwaka huu badala ya Februari 5 iliyozoeleka.

Alisema kuwa chama kimelazimika kubadili tarehe ya kilele ili kuwawezesha wananchi kushiriki ipasavyo maadhimisho hayo kwa kufanya kazi badala ya kuwa na sherehe mbalimbali.

“Maadhimisho ya safari hii ni tofauti na ya miaka mingine. Safari hii wananchi watatakiwa kushiriki zaidi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo. Kauli mbiu yetu ni ‘Sasa kazi’ hivyo watu wafanye kazi ili wajiletee maendeleo yao wenyewe,” alisema.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu jamaa ajui anachoongea

    ReplyDelete
  2. Ya kuvaa nguo za jeshi wakati si mwanajeshi
    Fyuuuuuuu
    Angalia waziri wa ulinzi alivaaa nini
    Kama angekwenda vitani angevaa nguo hizo siyo kwenye mahafari
    Pumbavu washauri wa rais Na CCM

    ReplyDelete
    Replies
    1. mgeni rasmi akienda kwenye mahafari ya chuo na yeye anakuwa ana graduate?
      akili za kuambiwa ongeza na zako shoga wewe la ukawa

      Delete
  3. Nape inaonekana unawashwa sana na upinzani?wakati wa kampeni umeisha boya wewe fanya kazi,wabongo wanawaangalia tu speed zenu hawataki sikia longolongo.

    ReplyDelete
  4. CCM mbele kwa mbele
    sema baba nape ni kazi yako kusema
    cheo chako kinarusi katibu wa itikadi na uenezi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad