Ni Nani Anayemdanganya Edward Lowassa? Mwacheni Basi Akachunge Ng'ombe wake Monduli!

Dunia inatambua Lowassa ana utajiri wa kifikra kuhusu njia ya kuwa fisadi nchini Tanzania. Kinachoendelea kwa sasa kinadhihirisha Lowassa anahitaji huruma za kisiasa kutokana na mwenendo wake kisiasa. Anahitaji sana ushauri usio wa kinafiki kuhusu hatima yake kisiasa nchini.

Nilivyomsikia kwa mara ya kwanza akitoa madai kuwa ukimya wake baada ya Uchaguzi Mkuu umesababisha kuwepo amani nchini, nilidhani kinachomsumbua ni mihemko ya kisiasa.

Nilipomsikia pia kwa mara ya pili akitamka maneno hayo Mkoani Arusha wakati akishiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Jimbo la Arusha ambao uliahirishwa katika siku ya Uchaguzi Mkuu baada ya kifo cha mgombea wa ACT-wazalendo Estomih Mallah sikushangaa sana.

Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipomuona tena kwa mara ya tatu ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Monduli akisema kunyamaza kwake baada ya wananchi kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kumewafanya wananchi wasiuane. Eti anadai wananchi walikuwa wanasubiri neno lake ili waingie barabarani na kuanza kuuana.

Lowassa anataka kutuambia watanzania wengi ni kama nyumbu kwamba kila atakalolisema watalifuata au kulitenda. Anataka kutuambia watanzania wengi wanafanya mambo yao kwa kutegemea kauli zake. Anadhani yale aliyokuwa anayaita mahaba kwenye mikutano yake ni unyumbu.

Hawa watu wanaomshauri Lowassa waache kumdanganya. Kuna baadhi ya watu wanamjaza ujinga ili adhani ana hekima na busara zaidi ya Watanzania wengi.

Lowassa na wapambe wake hawafahamu kama watanzania wengi wana haiba ya kutopenda vurugu. Hafahamu kama kuna chaguzi kuu nne zimefanyika na Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani na kuheshimiana. Hafahamu utawala wa machifu uliokuwa na nguvu kubwa (powerful influence)katika jamii nchini ulipigwa marufuku na Tanzania ikaendelea kuwa na amani na kuheshimiana. Hafahamu tuna makabila zaidi ya 120 yenye imani za kidini tofauti lakini yanaishi katika msingi wa kuheshimiana na undugu.

Lowassa na wapambe wake wangetafuta kwanza uzoefu kuhusu haiba ya Watanzania kutoka wapinzani ambao wamekuwa katika uwanja wa upinzani kabla yeye hajawaza/kufikiria kama kuna siku atakuja kuwa mpinzani wa serikali ya CCM.

Kinachoonekana kwa sasa Lowassa yuko katika safari ya kisiasa ambayo Augustino Mrema amepitia! Lowassa has gone from hero to zero! As a politician, he is finished. There is no way back for him.

Ni nani anamshauri Edward Lowassa? Mwacheni akachunge ng'ombe wake Monduli!

By MsemajiUkweli-JF

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. from hero to zero?
    nah..he never been a hero
    lowasa ni mbinafsi na mbaguzii

    ReplyDelete
    Replies
    1. FISADI NYANGUMI
      HABARI YAKE 'KWISHNEY'

      PPIIIIPPOOOZZZ PWAAAAAAA!!

      Delete
  2. Sijakuelewa wewe mtoa mada nataka kujua wewe uko wapi naona kama upo upande wa pili. Aidha kufilisika kwa lowasa kisiasa is none of your business lakini pia inakuuma nini? wewe kama hujui siasa za Tanzania basi heri unyamaze lini mrema alikuwa mpinzani mbona siku zote ni mfanyakazi wa serikali kama hujui kaulize. Hata Lowasa na sumaye bado ni wafanyakazi wa serikali wewe utahangaika wenzako wanakula mbuzi. utashangaa na roho yako kama utafuatilia siasa badala ya kutafuta mlo wa watoto wako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad