Profesa Mwesiga Baregu Amvaa Magufuli..Amkosoa Vikali Uteuzi wa Viongozi Alioufanya

Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu amekosoa uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu alioufanywa hivi karibuni na rais John Magufuli.

Profesa Baregu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema kuwa anaushangaa uteuzi huo kwani unakinzana na dhana yake ya kutaka kupunguza ukubwa wa serikali yake.

Tulitarajia kuwa rais Magufuli angechagua idadi ya makatibu wakuu ambayo inaakisi baraza lake la mawaziri, lakini nimeshangaa kuona kwamba kwenye baadhi ya wizara kuna makatibu wakuu wawili au watatu,” Profesa Baregu aliliambia The Citizen.

Aliongeza kuwa hivi sasa ni vigumu kufahamu kuwa nani atakuwa mtendaji mkuu kwenye wizara ambayo wameteuliwa makatibu wakuu wawili au watatu.

Naye Mkurugenzi wa Sheria katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia aliungana na kauli ya Profesa Baregu na kueleza kuwa ni vyema sasa sheria ikaweka ukomo cha idadi ya watu wanaopaswa kuteuliwa kwenye ofisi husika.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie wa ukawa au chadema haki ya kumkosoa mueshimiwa raisi mmeipata wapi? Kama si busara za watanzania sasa hivi tayari mlishamuweka muhujumu wa uchumi madarakani. Ukawa kabla ya kumkosoa magufuli mnatakiwa kumpa heshima yake kama raisi wa taifa la Tanzania. Mmemvunjia heshima na kulitia taifa aibu kule bungeni dodoma na kuendelea kujifanya mmepotoka kwa kutokuomba radhi halafu leo jeuri ya kumkosoa mueshimiwa raisi mmeipata wapi nyie watu msiekuwa na haya wala aibu. Haihalisi mtu profesa au mkulima ubora wa mtu unatokana matendo yake. Msitumie uprofesa wa majina kuuaminisha umma kwamba mnachokisema kina mshiko. Haingii akilini hata kidogo profesa mwenye kujitambua na kuheshimu taaluma yake kwenda kushiriki kupigania kumuweka madarakani mgombea wa uraisi mwenye kafsha ya upotevu wa mabilioni pesa za watanzania katika historia ya nchi hii? Muacheni muheshimiwa raisi afanye kazi yake watanzania tunamuamini na anachokifanya kwani hata kama muheshimiwa Magufuli angekuwa na baraza la mawaziri lenye mawaziri 60 au zaidi kama ilivyokuwa katika serikali iliyopita basi watanzania tunauhakika chini ya uongozi wa mueshimiwa magufuli nchi ingelipaa kimaendeleo kwani uzalendo wake na uchapa kazi uliotukuka ni kiwango wa kimataifa. Nnaomba radhi kusema hivi lakini sidhani hata kama kweli Tanzania ilistahili

    ReplyDelete
  2. Nyie wa ukawa au chadema haki ya kumkosoa mueshimiwa raisi mmeipata wapi? Kama si busara za watanzania sasa hivi tayari mlishamuweka muhujumu wa uchumi madarakani. Ukawa kabla ya kumkosoa magufuli mnatakiwa kumpa heshima yake kama raisi wa taifa la Tanzania. Mmemvunjia heshima na kulitia taifa aibu kule bungeni dodoma na kuendelea kujifanya mmepotoka kwa kutokuomba radhi halafu leo jeuri ya kumkosoa mueshimiwa raisi mmeipata wapi nyie watu msiekuwa na haya wala aibu? Haihalisi mtu profesa au mkulima ubora wa mtu unatokana na matendo yake. Msitumie uprofesa wa majina kuuaminisha umma kwamba mnachokisema kina mshiko. Haingii akilini hata kidogo profesa mwenye kujitambua na kuheshimu taaluma yake kwenda kushiriki kupigania kumuweka madarakani mgombea wa uraisi mwenye kafsha ya upotevu wa mabilioni ya pesa za watanzania katika historia ya nchi hii? Muacheni muheshimiwa raisi afanye kazi yake watanzania tunamuamini na anachokifanya kwani hata kama muheshimiwa Magufuli angelikuwa na baraza la mawaziri lenye mawaziri 60 au zaidi kama ilivyokuwa katika serikali iliyopita basi watanzania tunauhakika chini ya uongozi wa mueshimiwa magufuli nchi hii ingelipaa kimaendeleo kwani uzalendo wake na uchapa kazi uliotukuka ni wa kiwango cha kimataifa. Niombe radhi kusema hivi kwamba sidhani hata kama kweli Tanzania ilistahili kupata kiongozi muadilifu kama maghufuli kwani jamii bado inaonekana kugubikwa na dhana ya kuishi kwa kutokuajibika ipasavyo katika kushirikiana na mueshimiwa magufuli kupiga vita umasikini katika kulinda rasilimali ya kutotumiwa na watu wachache waliokuwa na roho mbaya.

    ReplyDelete
  3. nikitoa maoni yangu wale wote wavivu wa kufikiri,mahayawani watasema UKAWA HUYU,KATUMWA NA LOWASSA,YAANI DEMOKRASIA TANZANIA IMENGIA DOSARI YA BARIDI,TENA BARIDI KALI.imetokea,kwa mara ya kwanza kabisa nchini,wizara moja ina mawaziri wa nchi watatu,makatibu wakuu watatu na manaibu katibu mkuu watatu.sijui lakini embu tutoe nafasi tuupime utendaji wao na hususani kuwaelewa jee wanasimamia nini na au wanachanganyana kimajukumu yaani utendaji unapandana.labda niseme tuu kwamba hii ni farsafa mpya,tuipe muda,ila,ila,ila naona kama ukubwa wa baraza unafanana na ule wa awamu ya nne yaani MZIGO MKUU WA KWANZA WA MATUMIZI MAKUBWA YA SERIKALI.ATAKAYENIITA MIMI UKAWA NAOMBA AKANIKATIE NA KADI YANGU. NAITWA P.P.PANGAWE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad