Rais Magufuli Akosolewa Kwa Kutohudhuria Mkutano wa Umoja wa Afrika, Ikulu yajibu

John Magufuli
Baadhi ya wanasiasa na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wamemkosoa Rais John Magufuli kwa kutohudhuria mikutano ya Kimataifa ukiwemo mkutano wa Umoja wa Afrika (AU), uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia hivi karibuni wakidai kuwa ulikuwa muhimu sana kidiplomasia.

Wameeleza kuwa mkutano huo wa AU uliofanyika siku mbili nchini Ethiopia ulikuwa muhimu sana kwa kuzingatia utamaduni wa mikutano hiyo kuwakaribisha viongozi wapya wa nchi wanachama.

“Kama Mkuu wa nchi, Rais Magufuli alipaswa kuhudhuria mkutano huo ili akutane na viongozi wenzake na kubadilishana nao mawazo. Nadhani hayuko sahihi kwenye hili,” Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya aliliambia gazeti la The Citizen.

“Kwa namna hii, Tanzania inapoteza mengi, taswira yetu inafifia kwenye ngazi za kimataifa. Kiongozi wetu anapaswa kuona umuhimu wa kuhudhuria kwenye vikao kama hivyo vya kimataifa vya ngazi za juu,” aliongeza Mgaya.

Naye mhadhiri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco) ambaye ni mtaalam wa masuala ya kisiasa, Profesa Gaudence Mpangala aliunga mkono na kueleza kuwa mkutano huo ulikuwa na umuhimu sana kwa Rais Magufuli kuhudhuria akiwa na ujumbe wa viongozi wachache.

“Kama Rais Magufuli amepanga kupunguza gharama, angeenda na watumishi wachache. Lakini mkutano huo ulikuwa muhimu sana kwake na Taifa,” alisema Profesa Mpangala.

Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa alieleza kuwa Rais Magufu  alimtuma Makamo wa Rais, Bi. Samia Suluhu kuiwakilisha nchi kwa kuwa alikuwa na majukumu mengine nchini. Kwahiyo nchi iliwakilishwa vyema kwenye mkutano huo.

“Kama Rais hakuhudhuria ina maana alikuwa na majukumu mengine. Lakini aliwakilishwa na Makamo wa Rais. Kwahiyo kila kinachohusu Tanzania kitafanyiwa kazi ipasavyo,” Msigwa aliliambia gazeti la The Citizen.

Aidha alisema kuwa bado kuna mikutano mingi ya Umoja wa Afrika mbeleni ambayo Rais Magufuli atahudhuria.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hana mpango
    Tutamuona wa maana pale atakaposema ya Zanzibar

    ReplyDelete
  2. Hao wanaomlaumu raisi kwa kutohudhuria huo mkutano huko Ethiopia wakati wakijua kabisa kuwa Tanzania imewakilishwa tena imewakilishwa vyema tu kwani anachokifanya maghuful ni kitu cha kupongezwa mno for empowering Tanzanian women in international arena, im expecting to see condemnation from the Tanzania women organizations for whoever think Bi Samia Suluhu participation in representation our nation in international meeting is not worth. I think shame on every one who don't see how far Tanzania is in respecting women by letting Bi Samia to attend the meeting how heroic action by our president?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Can you tell us. Which nation sent representative Among those nations who participate in the metting. Try to think deeply guys

      Delete
  3. kwani makamu wa rais hafai kuwakilisha??? angetumwa waziri hapo sawa lakini aliyekwenda kule ni mtu wa pili baada ya rais. au mnataka rais asafiri ili asiwatumbue, acheni hizo safari zipo nyingi na muda upo wa kutosha atasafiri mpaka mtamsema maana watanzania hamna jema.

    ReplyDelete
  4. Ukiwa na ufinyu wa mawazo hilo huwezi kuliona. Siyo lazima Rais aende kwani maana ya kudelegate power ni ipi. Sawa siyo yote anaweza ku delegate lakini kwa hili yuko sahihi kumtuma Mhe. Makamu wa Rais kumwakilisha.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad