Sarakasi Zaanza Tena Umeya Dar es Salaam...Uchaguzi Wahairishwa

HALMASHAURI ya jiji la Dar es Salaam imeahirisha uchaguzi wa meya wa Jiji uliokuwa ufanyike leo, mpaka hapo tarehe itakapotangazwa baadaye.

Mkuu wa Kitengo cha Itifaki na Uhusiano na Umma wa Jiji, Gaston Makwembe alisema uchaguzi huo uliokuwa ufanyike leo saa nne asubuhi katika ukumbi wa Mmikutano wa Karimjee, umeahirishwa.

Alisema tarehe ya uchaguzi huo itapangwa baadaye na taarifa zitatolewa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari bila kueleza sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.

Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na mvutano wa aina yake kati ya vyama vinavyounda na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Diwani wa Kata ya Vijibweni, Isaya Mwita (Chadema) ndiye atapeperusha bendera ya Ukawa huku mgombea wa nafasi ya Naibu Meya akitarajiwa kutoka CUF. Chama Cha Mapinduzi (CCM ) wakiwakilishwa na Diwani wa Kinondoni, Yusuph Omary Yenga.

Inaelezwa kuwa Ukawa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti hicho kutokana na kuwa na idadi kubwa ya madiwani ambapo wanaizidi CCM kwa jumla ya madiwani 13.

Ikiwa Ukawa watafanikiwa kutwaa jiji hilo, itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa wapinzani kuliongoza tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

Awali, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alitoa mwito kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kusimamia uchaguzi huo kwa amani na haki ili usifanyike kama wa kumtafuta meya wa Ilala na Kinondoni uliokuwa na mizengwe mingi.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CCM vaaeni nguo za jeshi kwenye uchaguzi

    ReplyDelete
  2. Huyu zamaradi ya jiji yanamhusu nini
    Mbona ya mwanza, Arusha ,mbeya haonekani
    Watu kubebana
    Magufuli haya ndo majipu tusiyoyataka
    Kisa mtoto wa Kawawa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad