Serekali Yatangaza Kusitisha Matangazo ya Bunge Laivu Kuanzia Jana..Sababu Hizi Hapa

Serikali yatangaza leo Bungeni kuwa kuanzia tarehe 26 Januari 2016 TBC imesitisha kuonyesha baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge, kutokana na bajeti finyu.

Baada ya tamko hilo wabunge wa upinzani walipinga na kusimama na kupelekea bunge kuhairishwa

Soma, Zaidi

Mheshimiwa spika,
Naomba kutoa kauli ya serikali kuhusu TBC kutangaza moja kwa moja vikao vya majadiliano ya bunge. Mheshimiwa spika, shirika la utangazaji Tanzania, TBC lilianza kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2005. Kabla ya kuanza kurusha moja kwa moja, TBC wakati huo televisheni ya taifa ilikuwa inarekodi matukio yote ya bunge na kurusha usiku katika vipindi maalumu vilivyojulikana kama bungeni leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika.

Baada ya kuanza kwa utaratibu wa kuanza kurusha matangazo moja kwa moja mwaka 2005, gharama za kufanya kazi hio zimekua zikipanda kwa kasi hadi kufikia Tshs. bilioni 4.2 kwa mwaka kwa maana ya mikutano minne ya bunge.

Shirika limekuwa likigharamia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo madogo ya biashara, ifahamike kuwa asilimia 75 ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia 25 ni burudani.

Mheshimiwa spika, kutokana na hali hii, TBC imeona ni busara kubadilisha mfumo wa utangazaji wa shughuli za bunge ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za uendeshaji, hivyo basi, TBC imeona ni busara kuanzia mkutano huu wa bunge iwe inarusha baadhi ya matangazo ya bunge moja kwa moja yaani live ikiwa ni njia ya kubana matumizi.

Chini ya utaratibu huu, TBC itahakikisha kuwa, baadhi ya matukio ya matukio ya bunge yatarushwa moja kwa moja na mengine kurekodiwa na kuandaliwa kipindi maalum kitakachoitwa leo katika bunge. Kipindi hiki kitakua na mambo yote muhimu yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika. Kipindi hichi kitakuwa kinarushwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku.

Na mheshimiwa spika kipindi hicho kimeanza jana na tayari baadhi ya wananchi wameonyesha kuridhishwa na utaratibu huu na kuwa na kipindi maalum usiku kikishughulikia shughuli za bunge, mheshimiwa spika, uamuzi huu utapunguza gharama za uendeshaji

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. haaaaaaata!!! hiyo siyo sahihi na haikubaliki kwa UMMA. Ni juzi tu Waziri amewataka TBC wabuni njia za kuongeza mapato yao (Matangazo ya kibiashara),kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na hili? Mataifa mengi yalichukulia mfano huu uwe wa kuigwa kwa nchi zao leo hii sisi tunarudi miaka 10 nyuma.Tunapongeza hatua za serikali yetu kubana matumizi kwenye taasisi zake lakini kwa hili,mmetukatili sana wananchi wengi.

    ReplyDelete
  2. oooh mungu wangu,nape nnauye uwezo wa serikali ni mdogo au uwezo wa tbc ni mdogo?serikali leo hii inaona uchungu mkubwa wa tbc kutumia billion 4.2[kama ni kweli]kwa huduma hii muhimu kuwafikia watanzania kila kona ya nchi,hii ni kali nyingine isiyo kifani toka mamlaka ya serikali hii ya awamu ya tano,tunahesabu.kwanza ilikua ni kulifungia gazeti la mawio milele!wananchi tulio wengi kwa tanzania ya leo tumeweza kushiriki siasa,tena kwa wingi ambao nchi haijawahi kushuhudia.ushiriki huo ulikua ni UPIGAJI KURA WA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA ULIOFANYIKA JUMAPILI TAREHE 24 OCTOBA 2015, TUKACHAGUA.PAMOJA NA KUTOKEA YALIYOTOKEA LEO HII UWAKILISHI WA WABUNGE WA UPINZANI UMEPANDA TOKA 86 [ BUNGE LA 2010-2015]HADI KUFIKIA WABUNGE 124[BUNGE LA 2015-2020]ONGEZEKO KUBWA LA WABUNGE 38 WA UPINZANI.SASA ANACHOKIFANYA NAPE NI JARIBIO LILILOKWISHA SHINDWA LA KUZOROTESHA MAKALI YA WABUNGE WA UPINZANI KUSIKIKA KWA WANANCHI WAKIYAKOSOA MAPUNGUFU YA SERIKALI AMBAYO NI MENGI MNO.NI AIBU KUBWA SANA KWA SERIKALI YETU MPYA.KWA CHUKI HIZI AMBAZO NI MATOKEO YA SEMINA ELEKEZI YA WABUNGE WA CCM,JIANDAENI KUSHINDWA VIBAYA UCHAGUZI UJAO WA 2020.WANANCHI TUNASHUHUDIA.

    ReplyDelete
  3. Waache wazidi kuwapa wapinzani nguvu . nape na Riziwan ndio watu walikiua chama cha ccm.magufuli endelea kumbeba nape miaka mitano mtaendelea kuisoma namba

    ReplyDelete
  4. Bana matumizi hii sasa tusijeambiwa kunya Mara moja kwa wiki tusije jaza choo hasa vyoo vyetu vya serikali Tisha mnooo tunataka news Yale mapinduzi yt ya bunge moja kwa moja

    ReplyDelete
  5. MIMI namsikitikia Nape bado asubuhi kaingia na chuki ya u ccm dhidi ya upizani pole sana mh. Nafikiri hufai kuwa kiongozi wa taifa hili. Kumbuka upizani sio dhambi. Lakini kuiba na kufisadi mali ya umma ni dhambi kubwa ambayo baba wa Taifa analinganisha na ukoma. Leo hii unazungumza kubana matumizi kwa kumnyima mtoto wa miezi miwili maziwa eti na bana matumizi poor man shame on you. Sikia wewe waziri, Tunataka kusikia jinsi unavyotoa hoja tukupime kama sio wewe wenzako maana 2020 ipo karibu. Tunataka kujua kama wewe ulipita kihalali. Acha utani wako bungeni hapo sio mahali pa ccm peke yao. Kumbuka usemi wa Rais sasa uchaguzi umekwisha hapa ni kazi tu. kazi tu sio kuzuia habari bali ni kufanya kazi kwa maendeleo yetu, habari ni moja ya maendeleo rudi darasani Nape usione aibu.

    ReplyDelete
  6. Hivi, jipu linaitweje kwa lugha ya kigeni (a.k.a kiingereza)?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad