Serekali Yatoa Tamko Kuhusu Dawa Mpya ya Ukimwi Iliyogundulika Hivi Karibuni

SERIKALI imesema kama Shirika la Afya Duniani (WHO), litapitisha matumizi ya dawa mpya ya ugonjwa Ukimwi wataitumia, lakini kwa sasa haiwezi kuzungumzia tafiti za ugonjwa huo ambazo zipo nyingi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John, amesema kwa sasa zipo tafiti nyingi, lakini wao kama wizara wanasubiri mwongozo kutoka WHO ambao ndiyo unathibitisha ubora wa dawa na matumizi yake.
“Zipo tafiti nyingi tunazisikia zinafanyika, lakini hili la Ukimwi ni mapema mno kulizungumzia ila kinachohitajika ni kusubiri mwongozo wa WHO ambao ndio wanatuongoza kwenye orodha ya dawa na matumizi yake katika magonjwa mbalimbali,” alisema John.
Juzi mashirika mbalimbali ya habari yalitoa taarifa juu ya utafiti mpya wa dawa ya mseto ya kimiminika ijulikanayo kama PrEP ambayo inatarajiwa kuleta faraja kwa wenza ambao mmoja anaishi na virusi vya Ukimwi huku mwingine akiwa hana.
Dawa hiyo inadaiwa tayari imeanza kutumika kwa baadhi ya mashoga nchini Uingereza na Marekani ambapo huweza kuondoa hatari ya kuambukizwa hadi asilimia sifuri.
Pia itaondoa changamoto iliyokuwapo katika njia namba moja ikiwa pamoja na kujikinga na virusi vya Ukimwi, yaani kutumia kondomu wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Kutokana na matumizi ya kondomu wenzi hao walikuwa hawawezi kupata watoto bila uwezekano wa kuhatarisha afya ya mwenzi ambaye hana VVU.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. komeni ccm viongozi wote wa cmm ni waathirika
    kila leo india, ulaya kula dozi
    wasenge nyinyi dawa ni majaribio
    na bado bungeni umtakwisha wengi kwa ukimwi ccm

    ReplyDelete
  2. komeni ccm viongozi wote wa cmm ni waathirika
    kila leo india, ulaya kula dozi
    wasenge nyinyi dawa ni majaribio
    na bado bungeni umtakwisha wengi kwa ukimwi ccm

    ReplyDelete
  3. ukitaka mazishi ya kitaifa lazima uwe ccm
    sina kinyongo na marehemu
    lakini kama angekuwa cmm jeneza lingekuwa na bendera ya taifa
    huyu hakuwa kiongozi wa kitaifa tusitumie bendera only kwa watu fulani
    zanzibar wanasota leo RIP kisa karudi ccm na alikuwa mgonjwa miaka mingi
    na mlimwabia ccm lazima arudi ccm ili mazishi yake yawe ya kitaifa
    fuck u cmm

    ReplyDelete
  4. MATUSI YANAKUSAIDIA??? AU YANATUSAIDIA??? WATU KUWENI NA HOFU YA MUNGU. TOA COMMENT ZAKO KWA MAKINI. SIJAPENDA!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad