Mchezaji Mbwana Samatta aliyejishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa Ndani nchini Nigeria amezawadiwa na serikali kiwanja kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam na fedha taslimu ambazo kiasi chake hakijafahamika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.Lukuvi anayeonekana katika picha katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa serikali.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika hafla hiyo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine wengi wa serikali na wanamichezo.
Hahahahahahahaha!Admin kula ndimu.
ReplyDelete(Kwa nini Daimond hajapewa zawadi na serikali?)
ukumbuke yeye ni mwanamziki, nafiri kitu wanachokefanya sasa hivi nikuhamasisha vijana wafanye vizuri kwenye michezo na sio kukata viuono. Oops did i said that!!! yes tuataka vijana wafanye vizuri kwenye michezo.
ReplyDelete