Serikali Yasema Mawaziri Wakuu Waliokihama Chama cha Mapinduzi (LOWASSA na SUMAYE ) Wataendelea Kulipwa Pensheni Zao Kama Kawaida

Serikali imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM) wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi.

Mawaziri wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema)na badaye Lowassa aligombea urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji endapo watu waliokuwa katika nyadhifa hizo wanaweza kuzuiwa kuchukua pensheni zao kwa kuhamia upinzani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Angellah Kairuki amesema sheria haizuii kwa kuwa kuhama chama ni haki ya kikatiba.

Akinukuu Sheria ya mwaka 1999 pamoja na ile ya mwaka 2005 ya Utumishi wa Umma, Kairuki amesema waliokuwa viongozi katika nyadhifa hizo wana haki ya kuendelea kupata stahiki hizo kisheria.

Hata hivyo ameonya kuwa, wanapaswa kuheshimu sheria ya nchi inayowazuia kutoa siri za nchi wakati wakiwa katika nyadhifa zao.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, amesema uchumi ukiimarika utaisaidia serikali kuwalipa wastaafu pensheni itakayokidhi mahitaji yao.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naona aliyetoa hoja hii anafikiri atakaa ccm milele, nakuambia siku moja ccm itakuwa chama cha upizani kwa hiyo ukileta sheria za nyumbani kwako siku moja na wewe pensheni itakukimbia pole sana inaelekea wewe ni mbunge usiyependa kusoma sheria unaenda kusizia tu kama jamaa yangu mwaka huu hayupo mbungeni

    ReplyDelete
  2. KIJAJI JIFUNZE MAJIBU YA KINA.UNASEMA 'UCHUMI UKIIMARIKA WASTAAFU WATALIPWA VIZURI'.HILO SIO JIBU LA KWELI,NA SI SAHIHI KWA MTU MWENYE DHAMANA KUBWA KISERIKALI KAMA WEWE.NIKUKUMBUSHE SIKU ZOTE SERIKALI, KUPITIA KWENYE HOTUBA YA BAJETI YA MHE.WAZIRI WA FEDHA SERIKALI INATAMKA KUWA UCHUMI WA NCHI UNAZIDI KUKUA,NA PATO LA TAIFA LINAZIDI KUIMARIKA.WEWE KIJAJI UNASEMA AA UCHUMI WA NCHI UKIKUA.LINI?NAKUULIZA TENA LINI?ANGALIA KATIKA HOTUBA YA MAKADIRIO YA BAJETI MWAKA HUU WA FEDHA 2016/2017 WAZIRI WAKO WA FEDHA MHE,DOKTA MPANGO MSIKILIZE VIZURI HOTUBA YAKE KUHUSU UCHUMI WA NCHI.UJIFUNZE KWAKE.HIVI LEO KIJAJI HII 100,000 YAANI LAKI MOJA ANAYOPEWA MSTAAFU WA SERIKALI UPEWE WEWE SI ITAISHIA KWENYE KUNUNUA VOCHA ZA SIMU YAKO? NI FRACTIONAL PERCENT NGAPI YA MSHAHARA WAKO?MSTAAFU HANA MARUPURUPU KAMA WEWE YEYE NI STRICTLY SOLID LAKI MOJA.IMFANYIE NINI?MUWE CONSIDARATE.KAFAYA KAZI SERIKALINI KWA UAMINIFU MKUBWA MIAKA 40.SERIKALI IMEKULA UJANA WAKE WOTE,SASA BABU AU BIBI KOKORO.KISUKARI CHAKE,PRESSURE YAKE MANUNUZI YA DAWA YAKE,LISHE BORA HAPA SI YAKE,ATOE WAPI PESA.UPO WAPI KIFIKRA MHE KIJAJI AU NDIO KIATU KIKUBWA MGUU MDOGO?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad