Serikali Yatoa Picha Rasmi ya Rais wa Awamu ya Tano, Dkt John Pombe Magufuli

Picha Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli itaanza kuuzwa Januari 08, 2015, katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Mtaa wa Samora.

Kila nakala ya picha hiyo itauzwa shilingi Elfu Kumi na Tano tu bila fremu.  Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa shilingi Elfu Tano tu.  Aidha, Picha hizo zitauzwa katika Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Picha hizo zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za Umma, Mashirika na Ofisi binafsi.  Kila ofisi inatakiwa iwe na picha ya Mhe. Rais pamoja na Baba wa Taifa.

Serikali inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza  picha isiyo rasmi pamoja na Serikali kutoa taarifa kusitisha matumizi ya picha hiyo na wanaotengeneza picha ukubwa ambao siyo rasmi.

Hatua za kisheria  zitachukuliwa dhidi yao.  Idara ya Habari(MAELEZO) ndio yenye Haki miliki ya picha hiyo.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bumba claat!!..they could have done much better!! Mbaya kweli!!!!!

    ReplyDelete
  2. Hiki kizamadi ndo takataka gani hii
    Kupeana vyeo huku jakaya umetuaribia nchi
    Umeweka mizizi mibovu, majizi, mafisadi, wapumbavu, malofa
    It's will cost Tanzania 50 kutumbua majipu yote haya
    Mtu mwenyewe hata kuongea kwenye media hana mvuto, anamunyunga domo kama yupo kwenye taraabu eti msemaji wa serikali
    Magufuli anza na hawa tunataka vioo vya jamii ambao hawakubebwa na majina ya baba zao
    Kupumzisha ghasia ukuu WA wilaya mafia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad