Siku Moja Baada ya Kutolewa Kombe la Mapinduzi, Simba Wameamua Hivi Kuhusu Kocha wao Mzungu

 Uongozi wa klabu ya Simba usiku wa January 11 kuingia 12 unatajwa kufanya maamuzi magumu, kutokana na mwendo wa timu yao kwa sasa, stori kutoka mtandao wa mwandishi na mchambuzi wa soka Tanzania Salehjembe.blogspot.com, umeripoti uongozi wa klabu ya Simba kuamua kumfuta kazi kocha wake wa kiingereza Dylan Kerr.

Simba ambayo ilitolewa na Mtibwa Sugar katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2016 kwa goli 1-0, dalili za kuwa kocha Kerr yupo katika wakati mgumu, zilianza kuonekana baada ya afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara kufunguka kwa jazba kuwa yeye kama shabiki ameshangazwa na maamuzi ya mwalimu ya kutopanga mapema kikosi cha kwanza. Kerr anatajwa kuitwa kwenye kikao cha dharura lakini kikao ambacho kinatajwa kuwa tayari kina maamuzi.
Jackson Mayanja akisalimiana na Kerr wakati ambao alikuwa kocha wa Coastal Union ya Tanga.


Haji alikuwa akiongea baada ya mchezo akijitaja kwa kiasi kikubwa kama shabiki na sio kiongozi wa Simba, ili apate nafasi ya kutoa ya moyoni, hiyo ni moja kati ya dalili za Kerr kuwa alikuwa anawashiwa taa nyekundu. salehjembe.blogspot.com umeripoti nukuu chache za chanzo cha siri kuwa Kerr amefutwa kazi, nafasi yake itachukuliwa na Jackson Mayanja ambaye hivi karibuni alisaini mkataba wa kuwa kocha msaidizi, lakini sasa ataava viatu vya Kerr.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inaweza kuwa huyo coach huku ulaya ana licence ya kuwafundisha vichekechea na unajua ile kasumba ya sisi waafrika wengi ya kuwatetemekea wazungu kama vile wao ni miungu watu nayo inachangia sana kwa sisi waafrika kutojiamini kufanya mambo yetu bila ya kuwategemea wazungu umeishasikia/kuona kwenye hizi team za Ulaya coach toka Afrika?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad