Stori Kuhusu Mbwana Samatta Mara Baada ya Kutua Ubelgiji Kwenye Club ya Genk

Mbwana Samatta, amewasili nchini Ubelgiji tayari kujiunga rasmi na Klabu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Samatta aliondoka nchini juzi saa 6:00 usiku kuelekea Ubelgiji ili kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu hiyo mpya ya Genk, baada ya bosi wa TP Mazembe, Moise Katumbi, kukubali kumuuza.

Meneja wa mshambuliaji huyo, Jamal Kisongo, alisema amewasiliana na Samatta na kumweleza kwamba amefika salama na ameanza kufuata taratibu zote ili aweze kufanya kazi nchini humo.

Alisema mara baada ya kuwasili, alitakiwa kufuatilia kibali cha kazi ambacho kitamruhusu kufanya kazi katika klabu hiyo mpya na muda wowote ataanza mazoezi.

“Kuhusu Hati ya Uhamisho wa Kimataifa) (ITC), Katumbi (Moise) amemhakikishia kuituma kwa klabu hiyo, kwani kabla ya kuondoka juzi aliongea naye na kumpa baraka zote za maisha mapya katika Klabu ya Genk,” alisema.

Kisongo alisema kwa kuwa bosi huyo wa TP Mazembe ameridhia kumuuza Samatta kwa Genk, siku chache zijazo anatarajia kwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kusaini mkataba ambao atafaidika nao ikiwa mshambuliaji huyo atauzwa kwa klabu nyingine.

Samatta ambaye alitwaa tuzo ya kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, alikubali kujiunga na timu ya KRC Genk na kugomea ofa zilizotolewa na klabu za Nantes na Olympique Marseille za Ufaransa.

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Very good siyo GUD.....

    ReplyDelete
  2. Sidhani kama kwa kwenda kucheza Soka la kulipwa pale Ubelgiji kutamsaidia sana. Sioni kama ligi za Ubelgiji zinavutia sana katika kukuza kiwango cha wachezaji kama sio kuua vile viwango walivyokuwa navyo. Sana sana pale apatumie kama njia ya kwenda kwenye Nchi zenye ligi zenye msisimko wa hali ya juu na zenye kukuza vile viwango vya wachezaji, asiweke mkataba mrefu kama kuku anayetamia mayai (Ni Ushauri tu).
    Nadhani tatizo lingine ambalo anapaswa kulitegemea pale Ubelgiji, ni ile lugha, wale majamaa ni non - english speakers, kitu ambacho kitamletea upweke mkubwa na hatimaye kuudhoofisha uchezaji wake.
    Wakati mwingine ni muhimu sana kuzingatia ile Nchi unayokwenda kufanya kazi kuliko kukimbilia mahali kwa tamaa tu ya hela ama umaarufu. Akumbuke pale anapokwenda ndio itakuwa sejemu yake kimaisha, kwa hiyo maswala kama lugha ama kuwa karibu na washirika wenzako mtakaokuwa mnaelewana kiutamaduni ni muhimu sana.
    Kulinganisha na historia zilizopo, hayo mambo yamewakuta hata wale wachezaji maarufu kabisa hapa Duniani, ambapo baada ya ile mikataba yao kwisha waliamua kwenda kucheza kandanda kwenye zile Nchi ambazo hazikuwafanya wawe wapweke. Ama wengine ambao viwango vyao vilishuka kulinganisha na hizo sababu, mara tu waliporudi kwenye Nchi zao ama zile Nchi zinazofanana kiutamaduni na Nchi zao hali zao kimchezo zilirudi na kuwa bora kabisa.
    Sijui ni kwa nini Samatta hakushauriwa hivyo. Pengine ni kwa sababu ya pesa na pia kutafuta ule umaarufu ambao kimsingi kwa Nchi za Ulaya hiyo itakuwa kama Ndoto ya alinacha, kwani tutamsahau kabisa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fikra zako finyu basis wachina wasingekuja tz. Acha kukebehi juhudi za watu. Wanaocheza uingereza wrote wanajua kiingereza?

      Delete
  3. Kwa hiyo ulitaka akachezee Azam au yanga?mchezaji wa kiafrika anayetokea kwenye ligi za Afrika siyo rahisi kwenda moja kwa moja kwenye hizo ligi kubwa unazosema wewe..lazima apate daraja..hilo ndiyo tatizo mpaka leo hatuna wachezaji wa kutosha ulaya..unataka utoke simba uende chelsea moja kwa moja hiyo ni ndoto ya mchana..kuhusu lugha hilo wala siyo tatizo kama mchezaji wa kimataifa ni sawa na baharia wa meli tu unakuwa ushajiandaa kisaikolojia kuwa muda wowote unaweza kwenda popote,tupo hapa ubeligiji kama wenyewe mnavyoiita tulianza sifuri na hatukuwa na ndugu mpaka leo hii tuna familia halafu full happy..itakuwa samatta anayekuja kuanza kazi na mshahara juu..ashindwe mwenyewe tu...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad