Tamko la Star Tv, RFA Na Kiss Fm Baada Ya Kufungiwa Na Serikali Kwa Miezi Mitatu

Manejimenti ya sahara media group ambao ni wamiliki wa Star Tv, RFA naKiss Fm  imesema haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA  ya kutakiwa kufunga vyombo vyake.

Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 500 hadi kufikia mwezi October 2015.

Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA kanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.

Lakini menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutangaza kuvifungia vituo vyake kupitia mkutano wa  vyombo vya habari bila kujali athari zakufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.

Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.

Menejimenti pia imelaani taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki nakuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri jumamosi na jumapili sio siku za kazi.

Menejimenti ya star tv  inawaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake,  hatua  thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo hili kwa sahara media group limited  na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria, Kanuni Na Maridhiano.

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SAWA KABISA,TCRA NI TAASISI INAYOLIPISHA ADA ZAKE KWA DOLA ZA KIMAREKANI,HATA HIVYO ANKARA ZAO HALISI ZA KUANDIKA KWA MKONO(SIYO ZA EFD) ZINAONESHA SH. LAKINI WANAPOMWANDIKIA MTEJA WANATAKA WALIPWE DOLA

    ReplyDelete
  2. Iv hawa wa mwanza si ndo walikua na vihelehele vya kupga kampen mwaka Jana ..kila ukifungulia TV zao n lang za kijan na njano...
    fullll kurusha laivuuu kamoen ...
    hawa kupata ten pasent...haaaahaaaahaaaa haaaahaaa mwenzao Masanja kajirambia ten pasent za kampen nw anasukuma ki mnyama APA town..

    ReplyDelete
  3. Iv hawa wa mwanza si ndo walikua na vihelehele vya kupga kampen mwaka Jana ..kila ukifungulia TV zao n lang za kijan na njano...
    fullll kurusha laivuuu kamoen ...
    hawa kupata ten pasent...haaaahaaaahaaaa haaaahaaa mwenzao Masanja kajirambia ten pasent za kampen nw anasukuma ki mnyama APA town..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ha ha ha ha haaaaaa mbavu zanguuuuu uwiiii.... Makubwaaaaa

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad