Tusimruhusu Rais Magufuli Kusimika Utawala Wa Kidikteta Nchini- ACT Wazalendo

JANA limetokea tukio la aibu katika nchi yetu pale serikali ilipofanya jaribio la hatari la kuzuia wananchi kuona na kusikia kinachoendelea bungeni.

Kitendo cha serikali ya CCM kuzuia kuonyeshwa moja kwa moja vipindi vya bunge katika televisheni ya taifa ni cha kijima na sisi chama cha ACT-Wazalendo tunakilaani kwa nguvu zetu zote.

Tunakitafsiri kitendo hiki cha serikali kama mwendelezo wa hatua na juhudi za Rais Magufuli za kuminya demokrasia na kusimika utawala wa kiimla.

Tunawasihi wananchi kusimama imara na kuzipinga jitihada zozote ovu za kuminya demokrasia nchini.

Tunawapongeza wabunge wazalendo wa upinzani kwa kusimama pamoja na kupinga nia ovu ya serikali ya kuua demokrasia katika nchi yetu.

Tunawatia shime wabunge wote wazalendo kuendelea kupigania maslahi mapana ya taifa letu.

ACT-Wazalendo! Taifa kwanza leo na kesho!

Imetolewa na;
Samson Mwigamba,
KATIBU MKUU.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera sana wabunge WA upinzani

    ReplyDelete
  2. ASANTE ACT-MAENDELEO KWA MAONI YENU YALIYOJAA UKOMAVU MKUBWA WA KISIASA.NI KWELI KABISA TANZANIA YETU KWA VIASHIRIA VYOTE MUHIMU IMEKWISHA INGIA KWENYE UTAWALA WA KIMABAVU,UTAWALA WA KIDIKTETA.TUNAYASHUHUDIA MAZITO YA KULE BUNGENI,KAULI ZA WAZIRI MKUU MAJALIWA NA KAULI ZA MAWAZIRI.SASA HIVI CCM IMEAMUA ITUMIE NGUVU ZOTE ZA POLISI,KWENYE MEDANI ZA KISIASA KUZUIA MIKUTANO,KUZUIA MAANDAMANO,KUZUIA MAKUSANYIKO YEYOTE YENYE TAFSIRI YA KISIASA.KUNA NINI TENA HAPO KAMA SIO UTAWALA UNAOENDESHWA KIMABAVU,KIDIKTETA.HATUNA CHA KUFANYA POLISI WANAWAPIGA NA KUWADHALILISHA WABUNGE WETU AMBAO SISI TULIOWACHAGUA TUNAWAHESHIMU SANA NA KUWATHAMINI SANA.SIASA IMEINGIWA DOA TANZANIA SASA NI ENZI YA 'KAMATA,PIGA,WEKA NDANI.'

    ReplyDelete
  3. bila udikteka kidogo watu hawaendi

    ReplyDelete
  4. kwani hilo la udikteta ndio mnaliona leo, bado mtajutia mabao yenu ya mkono.

    ReplyDelete
  5. Tuacheni unafiki safari za nje Na allowance zilipokatwa mlishangilia kwa Sababu Ni za watendaji wa serikali. Sasa Ni zamu yenu hakuna kuuza sura Ni kazi Tu.

    ReplyDelete
  6. ATC Maendeleo mnatupeleka wapi mnataka mtusadikishe kwa unafiki wenu eti udikiteta igeni kasi ya Raisi wetu mpendwa kwa kuitakia mema tanzania na wananchi kwa ujumla nyinyi kubaniwa kuonyeshwa nyago zetu ktk tv tayari udikiteta wakati mlalahoi mlo mmoja kwa siku ni shida hamkuwahia kuituhumu serikali ya kidikteta wakati watu wanatafuna mabilioni ya pesa wacheni umbea watafutieni maendeleo watu waliowachagua sio kila leo ubishi usio kuwa na tija kwa watanzania mgepigania kipato cha chini cha mtanzania kwa siku kiwe dola 7 tungewaona wamaana hata mkitoka mjengoni kwa kupigania haki za watanzania

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad