Ubalozi India Tanzania Waingilia Maiti ya Mtanzania Kuzuiwa India

Ubalozi wa India nchini umeingilia kati sakata la kuzuiwa mwili wa Mtanzania, Abel Machanga aliyekwenda kutibiwa nchini India kabla ya kufariki dunia.
Mwili wa Machanga umezuiwa katika Hospitali ya Colombia Asia iliyopo kwenye mji wa Bangarole, hadi deni la dola 16,396 sawa na Sh 35 milioni litakapolipwa. Ufuatiliaji huo umekuja ikiwa ni siku moja baada ya gazeti hili kuchapisha habari kuhusiana na kuzuiliwa kwa mwili huo kwa siku 27 katika hospitali hiyo. Hivi sasa zinafikia siku 30.

Abel alifariki dunia Desemba 31 mwaka jana baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa kichwa aliogundulika kuwa nao baada ya kufanyiwa uchunguzi . Julai mwaka jana, gazeti hili lilichapisha habari ya maradhi ya kijana Abel hatua iliyosaidia kupatikana kwa dola 7,700 fedha zilizohitajika kwa ajili ya matibabu yake India.

Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa wa ubalozi, aliliambia gazeti hili kuwa taarifa hiyo imemfikia, Balozi Sandeep Arya ambaye ametaka kujua ilipo hospitali hiyo.

Balozi ameguswa na hiyo taarifa na kama inavyoonekana inaharibu picha ya India hivyo anataka kuifuatilia hiyo hospitali ingawa sijui ni kwa namna gani atalishughulikia suala hilo,” alisema

Ofisa huyo alieleza kuwa hospitali za Colombia Asia ziko nyingi nchini India hivyo inamlazimu balozi kupata anuani kamili ya eneo ambalo Abel alipatiwa matibabu na hatimaye kuaga dunia.

Katika hatua nyingine baba wa Abel, Revocatus Machange amesema mpaka sasa amepata takribani dola 16,000 ambazo ameshazituma nchini India.

“Namshukuru Mungu wasamaria wema wamesikia kilio changu nimeshatuma kiasi kikubwa cha pesa ninachosubiri kwa sasa mwili wake utolewe hospitali”

Kuhusu gharama za usafirishaji Machanga alisema anasubiri mwili wa Abel utolewe hospitali kisha masuala ya usafirishaji yatafuata baada ya kupimwa na kujua itagharimu kiasi gani.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inasikitisha sana....Mungu awape nguvu wafiwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad