Ukimkosa Prezzo Kwenye Muziki Ujue yuko Huku na Anaitwa Doctor Prezzo !!

Star wa muziki kutoka area code ya +254 kwa watu wa nguvu Kenya, rapper Prezzo japo hasikiki mara kwa mara lakini jina lake lipo kwenye majina ya wakali walioubeba muziki wa Kenya kwa kipindi kirefu toka ‘Genge’ yao ilivyopasua anga na kufahamika kimataifa.

Nimeipata Interview aliyofanyiwa siku chache zilizopita na mrembo Betty Kyallo Okari wa TV ya KTN ya Kenya… kaongelea mengi ikiwemo ishu ya kusomea udaktari.

‘Baba yangu alifungua Makini Herbal Clinic na mimi ni mtoto wa pekee wa kiume nyumbani, imenibidi nisome kuhusu masuala ya utabibu ili nisimamie shughuli za clinic… nitakuwa natoa huduma kwa watu na majaaliwa nitaitwa Dr. Jackson Makini. Nahitaji kuendeleza urithi wa kitu kizuri alichokijenga baba yangu‘- Prezzo.

Sentensi nyingine za Prezzo hizi hapa >>’Namkumbuka sana mzee wangu, angekuwa hai najua angejisikia fahari kuwa na mtoto kama mimi… nadhani angekuwa hata Rais wa Kenya‘- Prezzo.

Tazama Video Hapa:

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad