Umoja wa Vijana Chadema Wampa siku Tatu Rais Magufuli

BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kwa kushirikiana na Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu Chadema (Chaso) wametoa siku tatu kwa Rais John Magufuli kufuta agizo la Shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja mikutano ya Bunge inayoendelea Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi Taifa Bavicha Edward Simbeyi amesema, kitendo kilichofanywa na Serikali ni udikteta na kwamba, inawanyima wananchi kupata haki yao ya msingi.

“Tunajiuliza maswali mengi, ni vitu gani wanataka kuficha? Hadi wananchi wasivijue? Wakati Bunge linatakiwa kuwa masaa matano na dakika 45 sasa kwanini wanataka kurusha ndani ya saa moja? Haya masaa manne yanaenda wapi? Amehoji Simbeyi."

Amesema hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara yake ya 18 inatoa uhuru wa kila raia kupata au kupewa habari bila ya mashariti kama haya tunayoletewa leo.

“Wanaiogopa mijala inayoendelea Bungeni, Serikali yoyote inayoogopa kukosolewa lazima itakuwa na mapungufu yake, tunachohitaji ni mikutano uoneshwe live kila mtu ajue kinachoendelea” amesema Simbeyi.

Mbali na hilo, wameitaka serikali kutotumia ubabe ndani ya Bunge kwa lengo la kutaka kuwadhalilisha wabunge wa upinzani, pia Jeshi la polisi lizingatie maadili katika utendaji wao wa kazi na wasikubaliane na kila wanalotumwa na CCM hata kama linavunja sheria.

Amesema kitendo cha Jeshi la polisi kujiingiza katika masuala ya kisiasa ni kujidhalilisha wao wenyewe na ni hali inayoendelea kuwafanya kupoteza uaminifu wao ndani ya jamii.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Elimi finyu kwa polisi. Wanaamriwa. Na mkuu wa polisi labda hanui sheria za kaxi. Amezoea musema ndio bila kuea na uhuru pia. Polisi ni waleta na watunza amani. Awamu ilihopita ilikuwa ya kineshi sababu amiri neshi alikuwa mwananeshi kabla. Hakuweza kutenganisha kati ya neshi na raia. Yeya alikuwa ni salimu amri usiulze mimi ni kiongoxi. Udi tata wa bila elimu ndo huu .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad