Waliomkaidi Rais John Pombe Magufuli Waanza Kushughulikiwa

SAKATA la wafanyabiashara watano waliogoma kulipa kodi ndani ya muda uliowekwa na Rais John Magufuli limechukua sura mpya baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwakabidhi kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria.

John Maguli
Wafanyabiashara hao ni miongoni mwa 43 ambao awali walitajwa kupitisha makontena 329 bandarini bila kuyalipia kodi.

Mwishoni mwa mwaka jana, Rais Magufuli alitoa siku saba wajisalimishe wenyewe kulipa kodi kwa TRA bila adhabu.

Akizungumza na Nipashe ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo alisema kutokana na muda uliotolewa kuisha na wafanyabiashara hao kushindwa kutekeleza walichoagizwa vyombo vya dola vinaendelea        kulifanyia kazi suala hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Alisema wameamua kuvishirikisha vyombo vya dola kwa sababu wafanyabiashara hao wamekiuka agizo lililotolewa awali la kuwataka walipe kodi kwa hiyari yao ndani ya muda waliopewa.

Alisema makampuni ya wafanyabiashara hao, matatu yalichukua makadirio ya kodi wanayodaiwa na serikali lakini hayakwenda kulipa na mawili hayakuchukua kabisa.

Alisisitiza kuwa mpaka sasa fedha ambazo zimeshalipwa ni zaidi ya Sh. bilioni 11.9 ambapo wapo waliolipa zote na wengine kulipa sehemu ya malipo.
“Wafanyabiashara 19 wamelipa fedha zote walizokuwa wanadaiwa na wengine 19 wamelipa sehemu ya malipo, lakini wengine wamegoma wanahoji kulipa sehemu za adhabu,” alisema. “Mazungumzo yanaendelea kuhusu       wafanyabiashara hao.”

Mwishoni mwa mwaka jana, Rais Magufuli alitoa siku saba kwa wafanyabiashara hao kulipa kodi na kwamba mara baada ya muda huo kupita hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Makontena hayo yaliondolewa bila kulipiwa kodi katika Bandari Kavu kadhaa, ikiwemo ya Azam inayomilikuwa na mfanyabiashara Said Salim Bakhresa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad