Wananchi Waliobomolewa Nyumba zao Wacharuka..Watumia Mabango Kufikisha Ujumbe Kwa Rais Magufuli...


Wakati muda wa `mapumziko’ ya bomoabomoa ukimalizika leo huku jaribio la kupata zuio la muda likiwa limewekwa kiporo, wakazi wa Jangwani ambako nyumba zitaanza kubomolewa leo, jana waliweka mabango barabarani yanayotuma ujumbe wa aina mbalimbali kwa Rais John Magufuli.

Bomoabomoa hiyo ilianza Desemba mwaka jana likilenga nyumba zilizojengwa kwenye Bonde la Mto Msimbazi, lakini lilisitishwa kwa siku 14 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5, mwaka huu kuwapa nafasi wakazi kuondoka kwa hiari yao kuokoa mali zao.

Wakazi wa Jangwani walitumia mwanya huo wa kusitisha ubomoaji, kufungua kesi Mahakama ya Ardhi kupinga kuondolewa maeneo hayo bila ya kupatiwa sehemu nyingine na kuwasilisha ombi za zuio la ubomoaji, lakini chombo hicho cha sheria kilikataa kubariki mambo hayo ya kutaka sitisho la bomoabomoa liendelee wakati kesi ikiendelea mahakamani.

Wakati wawakilishi wa wakazi hao wakiwa mahakamani katikati ya jiji, watumishi wa halmashauri za jiji waliendelea kuweka alama nyumba zinazotakiwa kubomolewa wakiwa wamesindikizwa na ulinzi mkali wa polisi.

Hakukuwepo na wakazi waliojitokeza kuzuia uwekaji alama hiyo ya “X” inayotaarifu kuwapo kwa ubomoaji, lakini mabango ya maboksi yaliyosimikwa kwenye vifusi na maeneo mengine ya jangwani, yanatosha kuelezea hisia za wakazi hao wanaoishi maeneo ambayo yametangazwa kuwa hatarishi.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwanza kabisa napenda kuanzia na kusema maeneo mengi ya wazi nchini yalivamiwa kwa baraka za CCM
    Wanainchi walianza na kufunguwa matawi ya wakelekwetwa wa CCM viongozi wakuu wa ccm walifunguwa matawi haya kwa vishindo
    Watu wa kaanza kujenga sehemu hizi hasa Jangwani Dar , yakawa ni mazoea mafuriko yakitokea missada inatoka serikali ya ccm ikawa inatumia mabilion ya fedha , Tanzania tuna sehem kubwa sana ya watu kuuishi sasa kwanini wasitengeze maandalizi kwa watu hawa?
    Kabla , Kama ni uvamizi ccm ni namba moja maeneo mangapi nchini yalikuwa wazi CCM imejenga ofisi zao.
    Nafikiriki hata hayo mahekalu ni kulipiza kisasi tu ,
    Yatawagharimu sana haya ccm

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwahiyo wewe unataka waachwe hapo ili mafuriko yakija wafe sio,mbona wewe umekimbilia kibangu?

      Delete
    2. unafikiria kwa makalio sio bure wewe
      unataka waendeleee kusombwa na maji coz ccm ilijenga matawi. wamepewa viwanja mabwepande na mifuko ya cement na tofali wakaviuza thn wakarudi bondeni
      wahame tuu tena kwa bakora ikibidi acha serikali itumie nguvu ili badae waje kuisifia hata chini udikteta ulisaidia mpaka ipo apa ilipo sasa
      wahameeeeeeeeeeeeee bondeni

      Delete
    3. Kwani hamkujuwa wakati unafunguwa matawi ya wakelekwetwa au kwa sababu mnaishi masaki na Oyster bay

      Delete
    4. Mbona hamsemi makao makuu mlihamisha Dodoma tangu 1972
      Mbona hahamii huko CCM fyuuuuuuu
      Kila kukarabati ikulu kwa mabilion
      Tatizo lenu Kila mmeweka Dar ndo maana watu hawahawami Dar
      Hata ikulu ipo Dar makao ya inchi Dodoma shame you ccm fungeni domo lenu

      Delete
    5. we nawe pumba kweli umeng'ang'ana na ccm
      ccm ndo inakutawala wew ndo ufunge domo kaya lako ccm ikulete mabadiliko sio yale ya mikono zungusha haijalishi alifanya nini nyuma lkn sasa imefika mwisho wahame uko mabondeni wasijitie kuonewa
      watu kibao tumehama

      Delete
  2. SIO MUACHWE NA MAISHA YENU,MAFURIKO YAKITOKEA NYIENYIE NDIO MNABEBA MABANGO KUTUPIA LAWAMA SERIKALI KWAMBA HAIWAJALI.SWALA LA KUHAMA MABONDENI LIWEPO MUHIMU MUONYESHWE MAENEO.SIE WOTE TULIKUWA HUKOHUKO MABONDENI LAKINI TUMEHAMA NA MAISHA YANAENDELEA NA HAUNA HOFU HATA MVUA INYESHE YA MAWE TOFAUTI TULIVYOKUWA HUKO BONDENI.

    ReplyDelete
  3. Nimewasoma wote wachangiaji, lakini kuna jambop moja hamjaelewana. Serikali ni kama baba na mama katika hawa watu wawili mzazi mmoja anaweza kuwa mkali hataki mchezo na mwingine anapenda mizahaa. lakini wote ni wazazi! Lakini kuna jambo moja kwa mzaza wahenga walisema "Uchungu wa mwanae aujuaye mzazi" Hivyo basi uchungu huu wa bomoabomoa serikali inajua madhara yake kwa wananchi na faida zake pia. Hasara... watu wanalala nje na kung'atwa na mbu matokeo yake ni malaria..Faida... baada ya maumivu tutaingia katika nchi ya asali na maziwa. Jamani maumivu lazima yawepo. ndio maana wanasema mchumia juani atalia kivulini. Mwacheni tinga tinga afanye mambo baadaye tutafurahi wote.

    ReplyDelete
  4. eti nafsi izi zitakulilia mpaka kiama ??
    mtu mafuriko yanasomba nyumba yako yakiisha unatumia gharama kurekebisha na kujipanga upya then unakaa tena kwa wasi wasi coz unajua mvua zitakuja tena inaharibu mali zako then inauua kabisa familia yako wew kama kawaida yako unaingia gharama kurekebisha si bora huame ukaishi sehemu salama hata kama ni kijijin maisha popote sio lazima kuganda uko mabondeni kujitesa tuu kwa ujinga
    hata china inamkumbuka mao kwa maamuzi magumu aliyofanya na hata china imepiga hatua kimaendeleo mpaka hii leo na hata hivyo ni kwa faida yenu watanzania coz mafuriko yakianza mnakuwa wa kwanza kuitupia lawama serikali ukisahau kuwa hata wewe ni serikali pia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad