Wasira Kumrudisha Tena Esther Bulaya Mahakani..Sasa Kesi Kufunguliwa Upya Mahakama ya Rufaa

Steven Wasira
Baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza, kuipiga chini kesi iliyokuwa ikimkabili mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Esther Bulaya, wadai katika kesi hiyo wanatarajiwa kupinga uamuzi huo  Mahakama ya Rufani.

Akizungumza na Nipashe jana, mwanasheria wa wadai hao, Constantine Mutalemwa, alisema wateja wake hawajaridhika na hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Gwae.

Juzi katika mahakama hiyo, Bulaya aliwashinda wakazi wanne wa jimbo hilo waliofungua kesi ya kumpinga baada ya ushindi alioupata kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana. Katika uchaguzi huo, Bulaya olimshinda mpinzani wake, Stephen Wasira wa CCM.

Bulaya, katika kesi hiyo, alikuwa akitetewa na mwanasheria maarufu, Tundu Lissu.

Waliofungua kesi hiyo ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagira, ambao walikuwa na mawakili wawili ambao ni Mutalemwa na Denis Kahangwa.

Mutalemwa alisema baada ya kutoridhika na uamuzi huo, wateja wake wamekusudia kufungua kesi Mahakama ya Rufani ili kupata ufafanuzi wa Jaji juu ya uhalali wao wa kutokuwa na mamlaka kisheria ya kufungua kesi kama hiyo.

Katika hatua nyingine, kesi ya madai iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza na mbunge wa zamani wa Nyamagana (Chadema), Hezekiah Wenje, jana iliahirishwa hadi Februari 2, mwaka huu.

Uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo, ulitolewa na Jaji Joaquine De Mello wa mahakama hiyo, aliposikiliza kwa muda kabla ya kupangiwa jaji wa kuisikiliza kesi hiyo ya kupinga ushindi wa Stanslaus Mabula (CCM).


Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. heee ili babu vepe? alikubali kushindwa!!!

    ReplyDelete
  2. huyu mzee nae ndio wale wale akina membe
    ataki kukubali kama dogo amemzidi kete

    ReplyDelete
  3. Huoni Zanzibar.CCM.kwa miaka mingi inacheza mchezo mchafu, kuligi.

    ReplyDelete
  4. Ccm fyuuuuuuu
    Hata aibu
    Kwanza emehama nyumba ya serikali
    Au kauziwa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad