Watu 8 Wakiwemo Polisi Wafariki Dunia Kwa Kusombwa na Maji Kibaigwa Mkoani Dodoma

WATU 8 wamefariki dunia katika ajali iliyosababishwa na gari kusombwa na maji huku watu 6 wakiwa wa  familia moja.

 Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Davidi Misime amesema majira ya saa tatu usiku Jumapili, wananchi wa Kibaigwa walitoa taarifa jeshi la polisi kwa madai kwamba kuna gari limesombwa na maji na limetumbukia katika mkondo wa maji.

Amesema baada ya jeshi kupata taarifa hizo polisi walijitahidi kutoa gari hilo aina ya Rav4 yenye namba za usajili T516 DEP na kubaini kwamba jumla ya watu sita wa familia moja wamepoteza maisha katika familia moja.

Misime amewataja waliofariki kuwa ni Msaidizi wa Inspekta wa Jeshi la Polisi (IGP) Gerld Ryoba, mke wake Fidea Kihondo, watoto wawili binti wa kazi, na Koplo Ramadhani ambaye ndiye alikuwa anaendesha gari hilo.

Amesema wana familia hao  walikuwa wakitokea likizo mkoani Geita na walikuwa wakirejea kazini Dar Es Salaam.

Amesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Kibaigwa bwawani kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo ya Njoge, Embaemba, Kiteto na bonde la Ndurugumi.

Misime amesema gari hiyo ilikuwa limeharibika sana na walilazimika kulikata gari hilo na kuwakuta watu wanne ndani ya gari huku wawili wakiwa nje ya gari ndani ya maji.

Hata hivyo Misime amewataja watu wengine wawili wanaume  ambao walikutwa katika maji.

Kati ya watu hao wawili ambao ni wanaume amemtaja afisa mifugo kata ya Pandambili na anafahamika kwa jina moja la Ludege.

Amesema  mmoja mpaka sasa hajatambuliwa kwa jina huku madaktari wanafanya utaratibu wa kuandaa miili kwa ajili ya kuwasafirisha.

Amesema mtoto wa kazi aliyefamika kwa jina la Saraha atapelekwa Mbinga, Koplo Ramadhani anapelekwa Lindi huku miili ya watu wanne inapelekwa Geita.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad