Zari Hassan wa Diamond Aukacha Ukristo ! Atoa Tamko la Kuifuata Dini ya Baby Wake

BAADA ya sintofahamu nyingi kuibuka katika mitandao ya kijamii kuhusiana na picha za mpenzi wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zari the boss Lady, kusambazwa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akibatizwa mtoni, mwenyewe ameibuka na kuweka sawa sintofahamu hizo.

Akizungumza na mtangazaji, Millard Ayo kupitia kipindi cha Top Twenty, Zari alikubali kuwa picha hizo ni kweli zinaonyesha tukio la kweli la kubatizwa kwake lakini ilikuwa mwaka 2013 huku akishangazwa na usambazaji wa picha hizo kwa mwaka huu wa 2016.

“Nikweli nilibatizwa na kuwa Mkristu ilikuwa mwaka 2013, lakini sasa nina maisha mengine nimefuata dini ya mpenzi wangu, Diamond, nashangaa kwa nini picha hizo za mwaka huo ziwe stori leo wakati ni muda mrefu na sasa nina maisha yangu mengine,” alisisitiza Zari.

Aliongeza kwamba, licha ya kuwa na maisha yake mapya anaendelea na mambo yake mengine kwa kuwa yupo na maisha mapya hivyo anafuata dini ya mpenzi wake huyo ambaye ni maarufu na nyota katika muziki wa Bongo Fleva nchini huku akiwa na idadi kubwa ya tuzo zinazotokana na umahiri wa muziki wake.

Mtanzania

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani kwakuzaliwa yeye ni dini gani jamani? Au inategemea na mwanaume alonae kwa wakati huo!! Kazi kwelikweli!!

    ReplyDelete
  2. Na akikuacha ukipata mwingine kwenye dini tofauti utamfata.bi kizee wewe una mambo

    ReplyDelete
  3. akiwa kwa Ivan anakuwa mlokole, akija kwa Dai anabadilika ghafla anakuwa Muislam na kwakatunzi je xxxxx

    ReplyDelete
  4. mtu anaebadilisha Dini ni mnafiki sana. ni wakumuogopa!

    ReplyDelete
  5. Inamana yeye hanaga dini,ni bendera fata upepo! Hahahahaha majanga kweli kabisa

    ReplyDelete
  6. Inamana yeye hanaga dini,ni bendera fata upepo! Hahahahaha majanga kweli kabisa

    ReplyDelete
  7. Mamaa WA kuekeza namba zako tatu tatu alafu utasema nameshituka watanzania hamjui kingereza chali chalulah huna dini huna baba fyuuu

    ReplyDelete
  8. Hilo ZARI la kweli hajaki dini wala mungu anafuata uzuri wa maisha tu. AkioKota ZARI yeye hachagui.kutokana na sheria za ki Islam huyo anaitwa urtad na hawezi tena kuwa muislam Mpaka apigwe mawe hadi auwawe Ndipo atakasiki na huyo diamond jo sawa analala na nguruwe huyo ZARI hayuko tohara kutokana na sheria. Naamuepuka haraka kabla fimbo ya mungu haijamchapa6

    ReplyDelete
  9. Mmmmmh wadau kweli tumepata wifii na shemeji duh..napita jamani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad