Zitto Kabwe:Serikali Imekurupuka, Kuongoza Nchi Sio Kutumbua Majipu Tu

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kuonesha masikitiko yake kwa kitendo cha serikali kushindwa kuleta Bungeni mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano.
Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameweka wazi jambo ambalo serikali inapaswa kufanya baada ya uchaguzi na kusema ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

"Shughuli ya kwanza ya serikali baada ya uchaguzi ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano ( kutafsiri ilani yake kwenda kwenye mpango wa utekelezaji) . Bunge linapaswa kujadili na kuidhinisha Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 na kisha Mpango wa mwaka mmoja kuanza kutekeleza Mpango huo wa miaka 5. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT Ibara ya 63(3)(c), Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 hutungiwa sheria kwa ajili ya utekelezaji." Alisema Zitto Kabwe
 "Leo Serikali ya Rais John Magufuli ilipangiwa kuwasilisha Mpango huo wa Maendeleo wa miaka 5. Imeshindwa. Imeleta mwelekeo wa Mpango. Haikuleta sheria na Kamati ya Bajeti Imeleta maelezo yake kuhusu Mpango wa Maendeleo wa mwaka mmoja ilhali hakuna Mpango wa Miaka 5. 
"Mwenyekiti Chenge alitaka wabunge wajadili kwa mujibu wa kanuni ya 94 ambayo kimsingi ni Kanuni inayohusu Mpango wa mwaka mmoja. Serikali imejichanganya. Uongozi wa Bunge umechanganyikiwa." Aliongeza Zitto Kabwe
Zitto Kabwe alimaliza kwa kusema kuwa ni aibu kubwa kwa serikali inayojinasibu kwa kauli ya "Hapa kazi tu"

"Bunge linapaswa kuagiza Serikali ikalete Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 ili uidhinishwe na utungiwe Sheria kabla ya kuanza kujadili mipango ya mwaka mmoja mmoja.
"Ni aibu kubwa kwa Serikali ya ‪#‎HapaKaziTu‬ kushindwa kuleta Bungeni Mpango wake wa Maendeleo wa miaka 5 na hata ule wa mwaka wake wa kwanza. Itapangaje bajeti zake? Itatekeleza vipi ilani yake? Kuongoza nchi sio kutumbua majipu tu, ni kuendesha nchi." Alimaliza Zitto Kabwe.
Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole pole, Zitto. Mbona unakurupuka? Mpango wa Miaka mitano pamoja na majipu ni sawa na hakuna. Kwanza tusafishe majipu, baadae, hata kama mpango utaanza imebaki miaka miwili, shida hakuna. Ilmradi, HAPA KAZI TU!

    Aidha uwe macho, ACT-Wazalendo hawana uvumilivu kama CHADEMA. Ukiwatibua kwa miropoko yako hiyo, waweza kukutema ikingali asubuhi. Utaanzisha chama gani tena?!

    ReplyDelete
  2. serikali ya sasa hivi imekuja na sinema za matukio za kulaghai wananchi, hamna kitu magufuli kajitwisha u ccm hakuna jipya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anony 12:07 AM Wewe ni kichaa na sio vichaa wote wanavuo nguo hutambui ulisemalo soma wakati dear

      Delete
    2. Jamani wengine tunanyonyesha Na hizo hadithi zenu tunapenda ishu zinazomhusu ZITO lkn juu waraka nimesoma Mara sita kutokana Na time fupisheni tuu utaeleweka

      Delete
  3. Huyu Kaka kanichosha mpaka basi mnafiki

    ReplyDelete
  4. Hana lolote huyo, mbona mipango ya kuiba makontena bandarini hakuwahi kuisema?? Mbona mipango ya kuwalaza wagonjwa pale chini katika hospitali ya muhimbili hakuwahi kuisema???? Mbona mipango ya Serikali ya kuwalinda wezi wa nyara za Serikali hakuwahi kuisema???? Mbona mipango ya kuwafanya wanafunzi wa shule wakae chini kwa kukosa madawati hakuwahi kuisema???? Mbona mipango ya Serikali ya kuwaacha watu/wananchi wanaokaa mabondeni wafe na mafuriko hakuwahi kuisema???..............na mambo mengine mengi tu ya hiyo anayoiita mipango ya miaka mitano ya Bunge na Serikali zilizopita ambayo yameifikisha Nchi hii mahali iliko. Wewe Zitto Kabwe acha kuleta wanga hapa, wewe huna tofauti na mchawi. Miaka yoote hiyo huoni na wala umeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati. Bado kabisa hujui kuwa Watanzania wa sasa hatudanganyiki na hizo siasa zako za kutaka sifa na undumilakuwili. Wewe huyo huyo kwa mipango uliyokuwa nayo ulifukuzwa CHADEMA Chama Cha Wachagga na Dj Mbowe. Wewe huyo huyo na kwa mipango hiyo hiyo uliyokuwa nayo ulienda kuanzisha Chama Cha ACT - Wazalendo ambacho kwa mipango hiyo hiyo uliyokuwa nayo umeshindwa hata kupata Wabunge watatau(3). Leo hii bila ya aibu na wala chepe ya soni kwenye sura yako eti unahoji kabisa uhalali wa mipango ya Serikali hii tukufu ya JPM. Unashindwa kuona kazi kubwa iliyofanywa na hii Serikali kama ni sawa sawa na Serikali zote changanya na wewe katika miaka hiyo yote iliyopita........Wewe Zitto Kabwe ni mwanasiasa ambaye ni failure katika maisha ya kawaida mpaka maisha ya uanasiasa, huna lolote, umebakia na roho kuntu ya kwanini. Wakati Serikali ya Mtukufu JPM pamoja na Wananchi wenye moyo wa kujenga Taifa lao la Tanzania wanakimbia, wewe Zitto Kabwe na wenzako ndio kwaaanzaa mnajifunza namna ya kutambaaa, yani hata kusimama bado mnajishauri.........na pia usifikirie kuwa hatuelewi na wala usifikirie hatuna weledi wa kuelewa hayo maneno yako yanatokana pia kwa kunyimwa Uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mahesabu(PAC). Na bado, vijimaneno maneno vyako vitakutoka sana mwaka huu, na utaishia kuisoma namba wewe na wenzako. Ni ushauri tu tena wa bureee, nenda huko nje kakizatiti Chama Chako cha ACT - Wazalendo kabla hamjasoma namba, kwani #HAPAKAZITU

    ReplyDelete
  5. Ni kichekesho cha hali ya juu kuona wewe Zitto Kabwe na wenzako mnatuletea hoja dhaifu na zilizojaa uzandiki katika kuibana hii Serikali ya awamu ya Tano. Sisi kama Wananchi tulitegemea wewe Zitto Kabwe na wenzako mngetuletea hoja nguli za kuwakaba makoo wale wote wahujumu uchumi waliochangia kuifikisha Nchi hii mahali ilipo. Tulitegemea wewe Zitt Kabwe na wenzako mngetumia fursa hii kuwafungua macho Watanzania waliolala na kuwaeleza ni jinsi gani wanatakiwa kunyanyuka na kuzitumia vizuri zile fursa zinazotolewa na hii Serikali ya awamu ya Tano (SAT). Tulitegemea wewe Zitto Kabwe na wenzako kutumia vizuri hiyo fursa mliyoipata ya uwakilishi, kuwaelimisha Wananchi namna ya kukataa Rushwa na kujifunza kubana matumizi. Kwa kweli bila ya kumun'gunya sana maneno hizi zilizopo ni dalili tosha za kuishiwa kwa hoja kwa huyo anayejiita Zitto Kabwe na kundi lake. Sasa ninakuja kuelewa ni kwa nini ameshindwa hata kuwawakilisha vizuri wananchi wa jimbo la Kigoma. Huyu Zitto Kabwe ni Bomu ambalo ni zaidi ya jipu na mabalo linahitaji kutumbuliwa haraka sana. Anaturudisha nyuma sana Watanzania wa karne hii. Wakati sisi tunajaribu kujiimarisha kwa kutumbua majipu na kulinda rasilimali za Nchi zinazoliwa na wajanja wachache, yeye anajaribu kutufumba macho kwa kutuletea hoja zake ambazo kwanza, hazina mvuto wowote, na pili hazina mashiko..........huko ni kuishiwa sera, na kama ilivyo ada ya kuishiwa sera huyu Zitto Kabwe na wenzake sasa walichobakia nacho ni kupika na kupakuwa Majungu.

    ReplyDelete
  6. Anadhani serikali itaendeshwa na ubovu ulioachwa na aliepita majipu yatibiwe nfo mpango uwe
    Shida sisi siasa nyingi na ndo maana hatuendelei
    Kila siku tunaamka na tukio jipya

    ReplyDelete
  7. waambie zitto hao wanafikiri nchi inahitaji kutumbuliwa majipu tu., no, hapana kunahitajika hekima na busara zaidi ili kubalance mambo. sio timuatimua tu. magu atachemka tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. jidanganye hivyo hivyo nyie ndio majizi yenyewe waizi mpaka dawa mahospitalini
      unasumbuliwa na laana wew sio bure

      Delete
  8. wabunge wa upinzani wamazidi kuibeza serikali hawana lolote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad