Serikali imeamua kuondoa hoja yake ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano iliyokuwa imeuawasilisha mapema leo bungeni baada ya kudaiwa kuwa kilichowasilishwa hakikuwa mpango wa miaka mitano bali mwelekeo wa mpango wa mwaka mmoja.
Hatua hiyo imefikia baada ya wabunge Tundu Lissu na Zitto Kabwe kupinga mjadala wa hoja hiyo katika kikao cha leo mchana kuwa hakuna haja ya kuendelea na mjadala hadi serikali ipeleke mpango wa miaka mitano ukiambatana na muswada wa sheria husika.
Katika kikao hicho, ilipelekea mwenyekiti wa bunge Andrew Chenge kuahirisha kikao baada ya kambi ya upinzani kugoma kutoa maoni yake kupitia kwa mbunge David Silinde, na kupangwa kikao hicho kingeendelea jioni.
Katika kikao cha jioni, Mwenyekiti wa bunge amelazimika kuahirisha bunge hadi Jumatatu ijayo baada serikali kukubali kuondoa hoja yake kwa ajili ya kujipanga upya.
Zitto Kabwe na Tundu Lissu Waibwaga Serikali ..Sasa Yakubali Yaishe..Mpango wa Miaka 5
0
January 30, 2016
Tags