Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameilalamikia serikali ya Magufuli kwa kitendo chake cha kukaa kimya kuhusu ufisadi unaoendelea kufanywa na Harbinder Singh Seth, mmiliki wa IPTL, ambaye huvuna kiasi cha malipo ya bilioni 4 kila mwezi kama malipo ya kuliuzia umeme shirika la ugavi wa umeme nchini, Tanesco.
Zitto ambaye ni mmoja wa wabunge walioibua na kusimamia kidete sakata la ufisadi wa Tegeta Escrow bungeni mwishoni mwa mwaka juzi (2014), amesema hayo kufuatia tangazo la serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support ya miaka ya miaka 1980 na 1990s, ambapo ameisifu serikali kwa hatua hiyo na kuhoji iweje ikomae na kashfa hiyo tu, huku ikisita kuchukua hatua kwenye sakata la IPTL linaloigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kila mwezi isivyostahili?
Kampuni ya IPTL imeshalipwa fedha mara mbili tangu Rais Magufuli aingie rasmi madarakani, hivyo kufanya hesabu zitimie bilioni 8 kwa kipindi cha miezi miwili mpaka sasa.
Msome;
"Nimeona tangazo la Serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support. Hii ni kashfa ya miaka ya 1980s na 1990s. Ni hatua nzuri. Lakini ina maana gani wakati Serikali inavuta miguu kwenye suala la IPTL? Harbinder Singh Seth na genge lake wanavuta tshs 4bn kila mwezi. Kwa kutochukua hatua kuhusu IPTL, Rais Magufuli ameshaipotezea nchi mapato ya tshs 8bn tangu aingie madarakani. #TegetaEscrow ndio baba la mtandao wa ufisadi nchini kwetu" - Zitto Kabwe.
Zitto: Rais Magufuli Ameshaipotezea Nchi Mapato ya Bilioni 8 Tangu Aingie Madarakani
10
January 05, 2016
Tags
Sijui kwa nini tunaibiwa kimachomacho hatua haziness hukuliwi miaka yote
ReplyDeleteSamahani mdau ulietoa hiyo comment hapo juu mimi bado sijakusoma maana maneno yamepigana ngwara haieleweki unamaanisha nini
DeleteJamani mwacheni afanye kazi
ReplyDeleteHataki yamkute ya samaki wa Magufuli jamani ana watalaam wake wanafanyia kazi
Wakukaya fanya kazi
Huyu naye Zito kazidi Mwache magufuli afanye kazi kigoma inakusubiri hicho kiherehere sijui umerithi wapi kinakera
ReplyDeleteZito yupo sahihi na ninyi pia mko sahihi, unajua ufisadi ndani ya nchi yetu upo mwingi sana kwa hiyo inategemeana amechukua kablasha la nani siku hiyo. Tulieni wote waliofikiri TZ itaendelea kuwa shamba la bibi sasa basi. Zito sema ufisadi basi na ninyi wengine semeni kwa sauti ya juu kwamba ufisadi basi. Mwalimu alisema rushwa ni adui wa haki. kumbuka haki yako ya elimu, hospitali pamoja huduma nyingi tulishaanza kununua. sasa basi!!!!!!!inatosha....
ReplyDeleteNA HUYU ZITTO AMEKUWA MJINGA SANA
ReplyDeleteMwana ccm mwenzenu huyo kwa hiyo tulizeni vipapai vyenu
ReplyDeleteWana CCM na wengine ambao si Wana CCM hasa wale wenye maisha ya chini wanayo imani kubwa na utendaji wa Rais wao Mhe. John Magufuli. Kwa wenye wazo la kuifanya tanzania ipate maendeleo basi watoe ushauri kwa njia sahihi na si kuanza kutwishana lawama kama inavyoonekana kwa kijana Zitto.
ReplyDelete
ReplyDeletehakika yake.yaliyosemwa yanatimia
.
Zito naye yu kabila gn namuonaga tuu akikosoa wt hats sk moja hajasema well done kwa mtu yeyote
ReplyDelete