Zitto: Rais Magufuli Ameshaipotezea Nchi Mapato ya Bilioni 8 Tangu Aingie Madarakani

Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameilalamikia serikali ya Magufuli kwa kitendo chake cha kukaa kimya kuhusu ufisadi unaoendelea kufanywa na Harbinder Singh Seth, mmiliki wa IPTL, ambaye huvuna kiasi cha malipo ya bilioni 4 kila mwezi kama malipo ya kuliuzia umeme shirika la ugavi wa umeme nchini, Tanesco.

Zitto ambaye ni mmoja wa wabunge walioibua na kusimamia kidete sakata la ufisadi wa Tegeta Escrow bungeni mwishoni mwa mwaka juzi (2014), amesema hayo kufuatia tangazo la serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support ya miaka ya miaka 1980 na 1990s, ambapo ameisifu serikali kwa hatua hiyo na kuhoji iweje ikomae na kashfa hiyo tu, huku ikisita kuchukua hatua kwenye sakata la IPTL linaloigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kila mwezi isivyostahili?

Kampuni ya IPTL imeshalipwa fedha mara mbili tangu Rais Magufuli aingie rasmi madarakani, hivyo kufanya hesabu zitimie bilioni 8 kwa kipindi cha miezi miwili mpaka sasa.

Msome;

"Nimeona tangazo la Serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support. Hii ni kashfa ya miaka ya 1980s na 1990s. Ni hatua nzuri. Lakini ina maana gani wakati Serikali inavuta miguu kwenye suala la IPTL? Harbinder Singh Seth na genge lake wanavuta tshs 4bn kila mwezi. Kwa kutochukua hatua kuhusu IPTL, Rais Magufuli ameshaipotezea nchi mapato ya tshs 8bn tangu aingie madarakani. ‪#‎TegetaEscrow‬ ndio baba la mtandao wa ufisadi nchini kwetu" - Zitto Kabwe.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sijui kwa nini tunaibiwa kimachomacho hatua haziness hukuliwi miaka yote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Samahani mdau ulietoa hiyo comment hapo juu mimi bado sijakusoma maana maneno yamepigana ngwara haieleweki unamaanisha nini

      Delete
  2. Jamani mwacheni afanye kazi
    Hataki yamkute ya samaki wa Magufuli jamani ana watalaam wake wanafanyia kazi
    Wakukaya fanya kazi

    ReplyDelete
  3. Huyu naye Zito kazidi Mwache magufuli afanye kazi kigoma inakusubiri hicho kiherehere sijui umerithi wapi kinakera

    ReplyDelete
  4. Zito yupo sahihi na ninyi pia mko sahihi, unajua ufisadi ndani ya nchi yetu upo mwingi sana kwa hiyo inategemeana amechukua kablasha la nani siku hiyo. Tulieni wote waliofikiri TZ itaendelea kuwa shamba la bibi sasa basi. Zito sema ufisadi basi na ninyi wengine semeni kwa sauti ya juu kwamba ufisadi basi. Mwalimu alisema rushwa ni adui wa haki. kumbuka haki yako ya elimu, hospitali pamoja huduma nyingi tulishaanza kununua. sasa basi!!!!!!!inatosha....

    ReplyDelete
  5. NA HUYU ZITTO AMEKUWA MJINGA SANA

    ReplyDelete
  6. Mwana ccm mwenzenu huyo kwa hiyo tulizeni vipapai vyenu

    ReplyDelete
  7. Wana CCM na wengine ambao si Wana CCM hasa wale wenye maisha ya chini wanayo imani kubwa na utendaji wa Rais wao Mhe. John Magufuli. Kwa wenye wazo la kuifanya tanzania ipate maendeleo basi watoe ushauri kwa njia sahihi na si kuanza kutwishana lawama kama inavyoonekana kwa kijana Zitto.

    ReplyDelete

  8. hakika yake.yaliyosemwa yanatimia
    .

    ReplyDelete
  9. Zito naye yu kabila gn namuonaga tuu akikosoa wt hats sk moja hajasema well done kwa mtu yeyote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad