Adam Juma Aoga Matusi Baada ya Kuisifia Video ya Wimbo Mpya wa Ali Kiba ‘Lupela ’


Mtayarishaji mkongwe wa video za muziki nchini, Adam Juma Jumatatu hii amejikuta akishambuliwa kwa matusi katika mitandao ya kijamii baada ya kuisifia video ya wimbo mpya wa Ali Kiba ‘Lupela’.

Muongozaji huyo aliamua kumsifia Ali Kiba kwa namna kazi ya Lupela ilivyoandaliwa mpaka kukamilika.

Kupitia instagram, Adam Juma aliandika.
    Lupela @officialalikiba , this is art, watanzania hatujui kuidadavua art. Hatujui thamani ya kitu, tunachukulia kiurahisi urahisi tu, kila mtu anajifanya anajua kitu ambacho sio sawa. Hii sio video tu, tulia basi angalia kwa umakini utapata ujumbe usipoelewa inawekana tatizo lipo kwenye level yako ya kuchanganua ujumbe ktk picha, btw sio fan wa alikiba ni mwana tu. Ningependa kusema video ni A one, haifanani na kitu ambacho tumezoe!!! Go kiba

Hata hivyo baada ya ujumbe huo kukaa kutwa nzima ya jana, Adam Juma alirudi kwa mashabiki wake na kueleza kilichomkuta.

Kupitia instagram, Adam Juma aliandika : Jana nimeoga matusi mpk raha aisee….. kumbe ni hivi duu sikujua aisee.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad