AUDIO: Msikilze Hapa Rais John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa Maadhimisho ya siku ya Sheria nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma ya Sheria katika kushughulikia mashauri  yanayopelekwa Mahakamani.

Aidha amewataka Majaji na Mahakimu kutoa hukumu za mashauri  yanayowasilishwa Mahakamani kwa haraka ili kuwasidia wananchi wanaotafuta haki.

Akizungumza na mamia ya wageni kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya sheria, Dkt. Magufuli amewataka Majaji na Mahakimu hao kutanguliza Uzalendo na maslahi ya taifa mbele pindi wanapotoa maamuzi ya mashauri yaliyoko Mahakamani.

 Mhe. Rais amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  kuchukua hatua kwa watendaji wa Mahakama wanaokiuka maadili kwa kufanya vitendo vinavyochafua taswira ya Mahakama mbele ya macho ya jamii.

Aidha, Katika hotuba yake Mhe. Rais amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuijengea uwezo wa kifedha Mahakama ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Bofya  Hapa  Kumsikiliza  Rais  Magufuli  akihutubia

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jpm Hana masihara ingia kumi na nane zake uonje balaa lake,sasa hv tutaheshimiana Tu, Mara Mimi nafanya kazi TRA,TPA,cijui bank gani kumbe wezi, ILA sasa mnatusumbua kutukopa pesa ili mzibe ma gape mliyoiba kabla hamjatumbuliwa, thanx Mr President

    ReplyDelete
  2. Hasa wataesabu namba kazi mwaka mmoja nyumba gorofa mbili kiss nipo bank Fulani Wezi wakubwa

    ReplyDelete
  3. napenda kusikiliza Rais anapoongea jamaa anaongea ukweli tena kwa dhati kabisa
    Mungu mbariki rais wetu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad