Baada ya Lundenga Kukemea Matusi ya Mange, Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi Latoa Onyo

Wiki iliyopita kupitia mtandao wa Instagram,Blogger Mange Kimambi alimshambulia kwa matusi Aliyekuwa Miss Tanzania Hoyce Temu kwa kisa ambacho hata hakihusiani nae.Vilevile katika kashfa na tuhuma hizo walihusishwa hata watu wasiohusika katika ugomvi wa Mange na Ndugu yake Hoyce kinyume na sheria.

Hoyce Temu alieleza kusikitishwa kwake na maneno ya kashfa yasiyokuwa na chembe ya ukweli yaliyoelekezwa kwake na blogger huyo

Wadau mbalimbali walitoa maoni yao akiwepo Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga aliyelaani vikali tabia hiyo iliyofanywa na Blogger huyo kuchafua majina ya watu kwa kashfa na tuhuma za uongo kwa malengo yasiyoeleweka.

Alisema inasikitisha kuona mtu ambaye anaisaidia jamii kwa hali na mali akitungiwa kashfa za uongo na kuchafuliwa jina pasipo sababu yoyote ya msingi.

Vilevile waziri wa mambo ya ndani ameonya kuwa Jeshi la polisi litachukua hatua kali bila huruma na bila kujali mhusika alipo kwa wale wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya huku msemaji wa jeshi hilo akitoa msimamo mkali dhidi ya wale wote wanaotumia mitandao vibaya.

Amewataka wote ambao wanachafuliwa kwa njia ya mitandao waripoti TCRA au jeshi la polisi kwa hatua kali bila kujali jiografia ya makazi ya wahusika au mipaka.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hoyce na waliotukanwa na Mange wote wametumia uungwana sana kama mpaka sasa hawajafikisha bado kwenye sheria kitendo cha kutukwana vile.Mange wewe ni mama,kwa haya unayoandika kila kukicha unadhani unawafundisha kitu gani watoto wako/wetu?jirekebishe ndugu yangu,hivi hujiulizi kuwa watoto wako wakisoma haya unayoandika kama inawagharimu na labda kuwaumiza?Na ukisema hujali basi wewe sio binadamu wa kawaida,maana binadamu au mzazi lazima ajitambue.Ilikuwa mbaya,Acha.

    ReplyDelete
  2. huyo mange bora achukuliwe hatua maana amejiona yuko nje ya nchi hakuna wa kumfanya kitu , mshamba huyo nyumbani ni nyumbani usitapikie sahani unayolia chakula

    ReplyDelete
  3. Mange jamani ni mwehu kabisa anahitaji mabibabu. Kumsaidi ni apewe matibabu muhimu na ndo maana hata mzungu wake amechanganyikiwa kwa sasa hana msaada wowote toka kwa mke wake anajikuta hakijuta kila siku kuwa na mke kama Mange.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tunatakiwa tumuombee,Hakuna gumu kwa Mungu wetu.

      Delete
  4. Recho temu naye achukuliwe heka wala sio hatua na maombi yake inabidi yawe maalumu maana mtendwa akitendwa ndio inakuwa hivyo,,, Mange hajakurupuka tu kutukana Recho ndio aliye anza na ushaidi upo sasa mbona Mange ndio all over the news Recho je???? Ni ok kwake kutukana wenzake,,,,Think before make ur judgement.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mange ana jina kubwa TZ na kufuatiliwa na wengi sana ndio maana wengi tunamjua,binafsi huyo Recho ndio kwanza nimemsikia.Sijui kama unaweza kumfananisha Mange na Recho.

      Delete
  5. anatukanwa kikwete sembuse huyo nani sijui muelimishaji. acheni kijipendekeza kwani huyomuelimisha nini sijui ni mkuu kuliko amri jeshi mkuu JK au kwa kuwa huyo ni demu we......

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad