Baada ya Mkuu wa Wilaya Richard Kasesela Kutaka Kuzichapa na Mbunge Peter Msigwa...Maggid Mjengwa Afunguka Ukweli Kuhusu Kasesela

Niwe Mkweli Kuhusu Richard Kasesela..
Ndugu zangu,
Jana nilifika kata ya Mlenge, Pawaga mapema asubuhi. Niliongea na viongozi na wananchi walioathirika na mafuriko. Nilikuwa Mlenge saa tatu kabla ya Richard Kasesela hajafika.
Viongozi akiwamo Mtendaji Kata waliniambia DC Kasesela wamekuwa nae kila siku tangu mafuriko yatokee.

" Mheshimiwa DC anashinda na sisi kila siku kuanzia asubuhi mpaka jioni. Jana kaondoka saa kumi na mbili jioni." Anasema Sarah Mbilinyi, Mtendaji Kata ya Mlenge iliyoathiriwa sana na mafuriko.
Nikafika kijijini Kisinga kuliko na kambi ya wahanga wa mafuriko wanaotokea kitongoji cha Kilala kilichosombwa na mafuriko. Waathirika, wakiwamo akina mama na watoto wanamzungumzia vizuri Richard Kasesela wanayefyeka nae mapori na kujenga miundo mbinu mipya ya kitongoji cha Kilala Mpya ambao kuna wanaotaka kiitwe Kitongoji cha Kasesela.
Nikiwa hapo Kisinga, na ilipofika saa tano asubuhi nilimwona Richard Kasesela akiingia kambini hapo akiwa amevalia jeans, fulana na viatu vya raba.

Viongozi wa kijiji na wahanga walionekana kuwa karibu nae sana. Watoto wa hapo kambini walifurahia pia uwepo wake. Mara kadhaa alikatishwa kwenye mazungumzo kutokana na viongozi wa kitongoji, wahanga na watoto waliotaka kuongea nae.

Mimi siamini kabisa, kuwa Richard Kasesela anayafanya yale ya kule Mlenge kwa wahanga wa mafuriko na kwingineko kwa sababu ya kulinda U-DC wake. Nayaona akiyafanya kutoka kwenye moyo wake. Ni kiongozi wa kupigiwa mfano.
Nimetaka kuusema ukweli wangu kuhusu Richard Kasesela, kwa ninavyooamini mimi, basi.
Maggid,
Iringa

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tunajua viongozi wengi wanatafuta kiki hasa hao ma dc

    ReplyDelete
  2. Wewe maggid kwani anacholalamika msigwa ni nini?ni majungu ya huyo dc wako si kingine kwa nini yupo mdomoni mwa msigwa muda wote kwenye mikutano ya ccm?tatizo na wewe ni wale wale wa kijikomba ccm maggid.

    ReplyDelete
  3. Maggid huo sio ukweli na hauwezi kubadili yale tuliyoyaona na kuyasikia kwenye video clip. kwanza niseme wazi kuwa anafanya makosa makubwa kwenda peke yake bila kumuarifu na kufuatana na mbunge wa eneo hilo. anachokwenda kujaribu kukifanya na ambacho hakitafanikiwa ni kujaribu kumchafua mbunge aliyechaguliwa na wananchi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad