Barack Obama Asema Donald Trump Hawezi Kuwa Rais wa Marekani

Rais wa Marekani Barack Obama amesema anaamini mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani.

Rais Obama ameyasema hayo wakati wa mkutano mkuu wa kiuchumi wa nchi za kusini mashariki mwa Asia unaofanyika katika jimbo la California.

''Ninaendelea kuamini kwamba Bw Trump hatakuwa rais. Na sababu ni kwamba nina imani sana na Wamarekani,” amesema Bw Obama.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa Wamarekani hawatampigia kura Bwn Trump kwa kuwa wanajua kazi ya urais ni kazi kubwa si kazi ya kuongea na kuonekana kwenye vyombo vya habari tuu.

Kwa upande wake Bwn Trump amemjibu Rais Obana na kusema kuwa hakuna mtu aliyeharibu nchi kama kipindi chake.

Mwanasiasa huyo anamchukia sana Obama na miaka ya nyuma alizoea kumtaka atoe stakabadhi za kuthibitisha kwamba alizaliwa Marekani.

Chanzo BBC

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NINYI WATANZANIA ANGALIENI MARAISI WENU. SIASA YA KWENU IMEWASHINDA, SASA MNAFATA YA WAMAREKANI.....HATA KUPIGA KURA MAREKANI HAMUWEZI, BORA MNYAMAZE TUU!

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli kabisa ya zanzibar yametushinda tumeshikilia majipu. kweli obama urais si nchesho!

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad