Ben Pol Asema Kuchora Tattoo, Kuvaa Hereni na kufuga Rasta ni Mwiko Kwenye mwili wake

Msanii wa muziki wa R&B Benard Paul ‘Ben Paul’, amesema hapendi kuchora tattoo, kuvaa hereni pamoja na kusuka rasta kama baadhi ya wasanii wanavyofanya kwa kuwa ana uheshimu sana mwili wake.
ben-pol

Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Ben Paul alisema imekuwa ni kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii kujichora ‘tattoo’ na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake jambo hilo halina nafasi.

“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano wa tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwa sababu nauheshimu mwili wangu, ndiyo maana nipo kawaida kila wakati,” alisema Ben Pol.

Ben Pol na Jux hivi karibuni wameachia wimbo wao mpya uitwao ‘Nakuchana’.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi sana kaka na hizo cheni uzivae

    ReplyDelete
  2. Safi kabisa nakukubali, achana na hao wanaojifananisha na dada zao

    ReplyDelete
  3. safi sana kaka. cheni vaa hazina shida kabisa. hongrera sana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad