BAADHI ya baa zilizopo katika viwanja vya Legho, Ubungo jijini Dar, leo zimevunjwa kufuatia agizo la mahakama kwa kile kilichodaiwa wamiliki walivamia eneo ambalo siyo lao.
Akizungumza na mwandishi wetu, dalali wa mahakama kutoka katika kampuni ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd, Elieza Mbwambo, alisema mmiliki halali wa eneo hilo ni Dar Cool Makers Limited ambaye baada ya kuvamiwa eneo lake alifungua kesi mahakamani mwaka 1993 ambapo iliendelea mpaka ilipofikia leo.
Wavamizi wa eneo hilo ambao ni John Ondoro Chacha, Jumuiya ya Wazazi CCM na mtu mwingine mmoja baada ya kuona mmiliki halali amepeleka kesi mahakamani nao wakaenda kuweka zuio ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru eneo hilo lirudi kwa mmliki halali ambapo wavamizi walitakiwa wabomoe vibanda walivyokuwa wamejenga walikokuwa wakifanya biashara ya baa.
“Januari 25 mwaka huu tulipewa oda na mahakama tuje kuwatoa hawa wavamizi, tuliweka tangazo kama wiki moja iliyopita lakini hawakujali hivyo leo ikawa ndiyo siku rasmi ya kuwaondoa na kama unavyoona ndiyo tunabomoa hivi.
“Mwenye kesi ya msingi ambaye ni John Ondoro Chacha alitakiwa kuwaambia wapangaji wake kwamba ameshindwa kesi lakini hakuwaambia ndiyo maana hata tangazo lilipowekwa hawakushtuka, kwa mujibu wa mahakama huyu Chacha ambaye kwa sasa ni marehemu na watoto wake ndiyo walikuwa wakipokea kodi ya kila mwezi kwa wafanyabiashara waliowapangia wakati eneo hili siyo lao,” alisema Mbwambo.
Watu mbalimbali walionekana wakiwa wamesimama huku wakishangaa eneo hilo huku wengine wakilalamika kwamba watakuwa wanajiachia wapi wakati walikuwa wamezoea viwanja hivyo.
Source-Global Publishers
Bomoa Bomoa Zaikumbu Sinza...Baa za Uwanjani Legho Zavunjwa
1
February 05, 2016
Tags
Bora foleni lipungue sinza
ReplyDelete