Bunduki iliyotungua Helkopta na Kuua Mzungu yapatikana Simiyu.

Bunduki hiyo aina ya Riffle Na 7209460 CAR Na 63229, imepatikana mara baada ya jeshi la polisi kufanikiwa kuwakamata watu 9 wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda Lazaro Mambosasa amesema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA.

Aidha waliokamatwa wamekiri kuhusika na tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa ulifanywa na jeshi hilo mara baada ya tukio kutokea chini ya mkuu wa upelelezi mkoa Jonathan Shana.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi sielewi sijui! Angelkuwa Ruban mtanzania wangefatilia hili swala? Au ndio kusema kila kitu ni nimipango ya Mungu!!? Mengine sio kutumia akili kufkria!

    ReplyDelete
  2. Mbona mnashinwa kuweka nguvu kama hizi kwa raia wa Tanzania walipa kodi? Uwezo mnao, tatizo kutokumheshimu mtu mweusi? kutokujiheshimu mwenyewe na kutokujithamini. Wauza madawa vilevile Raisi anamajina ameyakalia miaka. Ni aibu kubwa. Inabidi tuwaulize kwa nini hamjithamini mpaka mzungu akukalie shingoni akudai na kukulazimisha? Hii inatia haya na mnajidharilisha ndo maana mnatumika na mataifa. Kisa Wanawajua udhaifu mlionao. mpaka mlazimishe. Au muonyeshwe pesa, .Utaifa hamna kabisa.Hii inakatisha tamaa kwenye karne ya 21 bado mtu mweusi hawezi kujitawala bila mzungu hata akipewa elimu anabaki kutumika tu. Inferiority complex.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad