Collabo ya Shilole na Nicki Minaj yanukia

Siku chache baada ya kuachana na Nuh Mziwanda, mwanadada Shilole ‘Shishi Baby’, kupitia account yake ya Instagram ametoa tangazo la kuomba msaada. Tangazo hili linasema

“Anatafutwa mwalimu wa kingereza mzuri, jamani huu sio utani nipo sirias naona hali ishakuwa sio hali soon natakiwa kuonaa na Niki Minaji hivyo lazima nijinoeee, namba ya sm 0653883839“, aliandika Shilole kwenye ukurasa wake wa instagram

Shilole anafahamika kwa kutojua lugha ya kingereza, hivyo kuwa gumzo anapoongea lugha hiyo ambayo mara kwa mara huwa anachapia, lakini cha ajabu yeye mwenyewe huwa anafurahia na hajutii kuzungumza lugha hiyo ambayo haijui, kama alivyowahi kutamka neno la “I love is my country“, ambalo lilikuwa maarufu na watu kuvutiwa nalo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad