Chama cha Wananchi CUF, kimesema hakitarudi kwenye meza ya mazungumzo ya kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani Zanzibar hadi mchakato wa uchaguzi mkuu wa marudio usitishwe.
Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hawawezi kuendelea na mazungumzo huku wenzao wakiendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu, na kwamba iwapo uchaguzi mkuu wa marudio uliotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kufanyika Machi 20 utasitishwa, chama hicho kitakuwa tayari kufanya mazungumzo.
Maalim Seif Sharif Hamad ametoa kauli hiyo leo jijini Dar e salaam, mara baada ya kukutana kwa mazungumzo na aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Edward Lowassa na kisha viongozi hao kuzungumza na waandishi wa habari.
Katika hatua nyingine wanasiasa hao maarufu nchini wameitaka serikali ya mapinduzi Zanzibar, kuchukua hatua za haraka kukomesha kile walichokiita hujuma wanazofanyiwa wafuasi wa upinzani visiwani Zanzibar.
Maalim Seif Shariff Hamad ambaye pia ni makamu wa kwanza wa Rais ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, amesema kumeibuka kundi la watu ambao wamekuwa wakivunja na kuiba mali za watu na kuondoka bila ya kuchukuliwa hatua zozote na vyombo vya ulinzi na usalama.
Mwandishi wa Channel ten alitaka kujua, yeye kama makamu wa kwanza wa Rais amechukua hatua gani kuzungumza na vyombo vya ulinzi na usalama ili kukomesha kile alichokiita hujuma kwa wafuasi wa vyama vya upinzani, kiongozi huyo ambaye pia ni katibu mkuu wa CUF Zanzibar anaeleza zaidi.
Pia ametuhumu serikali ya mapinduzi Zanzibar, kuwa imekuwa ikichukua na kunakili namba za vitambulisho vya mzanzibar mkaazi na vya mpiga kura vya watumishi wa umma , kwa kile alichokieleza kuwa ni kuwachukulia hatua wale ambao hawatashiriki kwenye zoezi la kupiga kura la Machi 20
Go maalim mpaka ccm wakae. hatuwezi kurudia uchaguzi kisa ccm wameshindwa.
ReplyDelete