Director Adamu Juma Afunguka..Akerwa na Wanamuziki Kwenda Kufanya Video nje..

Kupitia instagram, Adam Juma ameandika:

Katika hizi siku za karibuni kumekua na mwaswali mengi kuhusu wasanii kufanya kazi nje ya nchi, kila napopita swali ni hilo. Je kufanya kazi njee ya nchi ni sawa au si sawa? Jibu lake si rahisi na kiukweli linahitaji fikra kwa anayelijibu kulingana na nafasi yake. Industry ya mziki ni pana sana, katika upana wake imewapa fursa vijana wengi kufanya kazi na kujikomboa kimaisha, katika video kuna vionjo vingi sana ambavyo ni ajira kwa wengi, kwa mfano dancer na mavazi nk. Jambo hili kama nilivyosema awali usipo litafakari unaweza ukajibu kikawaida tu, ili industry ikue ushirikiano huu wa fani tafauti tafuti unahitajika sana.

Nakumbuka shows zamani zilikata zikaja Dar live mwaka mzima, ghafla ikawa bills na maisha, mpaka sasa jiii hamna kitu. Mdomo ukizoe mnofu mwishowe meno hugeuka kitoweo, show sikuhizi za kutafuta na haya yote ni madhara ya pupa. Wasanii wanaofanya video nje naamini wengi wanasababu za msingi ila bila fikra hawajui kinachotokea nyumbani, leo hii hakuna sababu mtu awekeze kwenye vifaa vya music video crew zinavunjika kila siku, models imekua story ndefu na mengine mengi yanajitokeza kila siku. Kinachosikitisha nipale unaposhot video ya $10000 alafu ukirudi nyumbani unalia na mil3 alafu watu wakiingia youtube director unanyewa kama mtoto wa kambo huku wakikulinganisha na director flani. Kweli kuna vitu wametuzidi lakini ubunifu nasie km watanzania tupo, tusitengeze mazingira siku moja tuje kushindwa kufanya kazi hapa nyumbani. Kuna faida nyingi za kushot njee tusijisahau, wanaija wameshtuka GOD anajua. Regards to all

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad